Rais wa Zimbabwe aunda kikosi kazi kushughulikia vurugu za baada ya uchaguzi
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameunda kikosi kazi kinachoshirikisha wizara tofauti ili kushughulikia masuala yaliyotajwa katika ripoti za hivi karibuni na matokeo ya uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu.
Waziri wa sheria na waziri wa mambo ya nje wameteuliwa kuwa mwenyekiti na naibu mwenyekiti wa kikosi kazi hicho, na wajumbe wengine ni pamoja na waziri wa habari, waziri wa fedha, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa viwanda, waziri wa usalama wa taifa, na wengine kutoka shirikisho la wanasheria na tume ya uchaguzi.
Kikosi kazi hicho kimetoa mapendekezo kadhaa yakiwemo kuitisha mazungumzo ya kitaifa kati ya vyama vikuu, kutoa fidia kwa waathiriwa, kuchunguza sheria zinazohusika na kauli za chuki, vitendo vya kutumia ovyo mtandao, na kuchochea vitendo vya kimabavu.
Wachunguzi wa kimataifa wameridhika na mazingira ya amani kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, lakini wamesikitishwa na vurugu zilizotokea tarehe mosi Agosti mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, na kusababisha vifo vya watu 6.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |