UN yasema Ebola imeenea kwenye "eneo la hatari kubwa ya kiusalama" DRC
Umoja wa Mataifa umesema mlipuko wa homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC si kama tu unaendelea kuenea, bali pia unaelekea kusini kwenye "eneo la hatari kubwa ya kiusalama" nchini humo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Shirika la Afya Duniani WHO limetoa ripoti likisema idadi ya watu wanaoripotiwa kuambukizwa Ebola mkoani Kivu Kaskazini nchini DRC imeongezeka ndani ya wiki chache za karibuni, hasa katika eneo la Katwa, ambako timu za wataalam wa afya zinakumbwa na kutoaminiwa kwa jamii.
Shirika la Afya Duniani limeshirikiana na taasisi husika za nchi hiyo kujenga uaminifu katika jamii, na kuimarisha hatua za kupambana na homa ya Ebola kwenye maeneo hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |