Tamasha la kusherehekea mkesha wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China lilifanyika Jumatatu usiku ukiwa ni mkesha wa mwaka huo mpya.
Tamasha hilo limeandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, na kutumbuizwa kwa nyimbo, ngoma, mazungumzo ya kuchekesha, mazingaombwe na sarakasi ambazo zimeonesha imani thabiti ya watu kutafuta na kutimiza ndoto ya China, na kueleza furaha na hisia ya kupata waliyo nayo watu wa China.
Tamasha hilo la mwaka huu ni la kwanza kufanyika baada ya kuzinduliwa kwa CMG, ambayo imetumia njia mbalimbali za vyombo vya habari na teknolojia mpya kama vile 4K, 5G, VR kulitangaza. Pia limeshirikiana na kampuni za Baidu na TikTok na kuchezesha bahati nasibu.
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni siku ya kujumuika kwa wanafamilia, ndiyo maana "familia", "upendo" na "neema" ni kauli mbiu muhimu ya tamasha hilo. Mwaka huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na pia ni kipindi kipya cha kuelekea utimizaji wa jamii yenye maisha bora.
Viongozi wa nchi mbalimbali wametoa salamu za pongezi kwa serikali ya China, wakieleza matumaini yao ya kuendelea kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na China.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kwenye salamu zake kuwa urafiki na ushirikiano kati ya Kenya na China ni wa muda mrefu, na katika miaka ya hivi karibuni nchi hizo zimekuwa karibu zaidi kwa kushirikiana katika sekta mbalimbali kutoka viwanda hadi miundombinu, jambo ambalo limebadilisha maisha ya watu wa kawaida wa nchi hizo mbili.
Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema kwenye tafrija ya mwaka mpya wa jadi wa China iliyofanyika katika makazi yake 10 Downing Street kuwa uhusiano kati ya Uingereza na China ni muhimu sana, na nchi hizo zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja ili kufanya ushirikiano wao upate mafanikio zaidi. Naye Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe ametumia kichina kuwatakia heri ya mwaka mpya watu wenye asili ya China na wachina waliopo nchini humo. Ameeleza matumaini yake kuwa uhusiano kati ya Japan na China utaendelezwa zaidi katika mwaka mpya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |