Rais Trump amteua naibu waziri wa fedha Malpass kuongoza Benki ya Dunia
Rais Donald Trump wa Marekani amemteua David Malpass, naibu waziri wa fedha wa Marekani anayeshughulikia masuala ya kimataifa, kuwa mgombea wa Marekani wa nafasi ya rais ajaye wa Benki ya Dunia.
Rais Trump amesema Malpass ni mtu hodari sana na "ametafuta kwa kina" mtu wa kuchukua nafasi iliyoachwa na Jim Yong Kim, rais wa zamani wa Benki ya Dunia aliyejiuzulu ghafla mapema mwezi Januari na kujivua majukumu Ijumaa iliyopita. Ameongeza kuwa Malpass ametetea sana wajibu wa Benki ya Dunia na kwamba amefanya juhudi kuhakikisha fedha zinatumiwa katika mahali na miradi ambayo kweli inahitaji msaada wakiwemo watu wanaoishi katika umaskini unaokithiri.
Malpass atalazimika kupitishwa na bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Dunia kabla ya kuweza kuongoza Benki hiyo.
Wagombea walioteuliwa na Marekani, nchi ambayo ni mmiliki mkubwa zaidi wa hisa wa Benki ya Dunia yenye mamlaka ya kupigia kura asilimia 16, wote hatimaye walifanikiwa kushika nafasi hiyo tangu Benki hiyo izinduliwe mwaka 1944. Utamaduni huo wa muda mrefuumekitilia mashaka kiwango cha kutegemewa kwa shirika hilo kwani michango iliyotolewa na makundi yanayojitokeza hivi karibuni na nchi zinazoendelea kwa ukuaji wa uchumi duniani imeizidi ile iliyotolewa na nchi zilizoendelea katika miaka ya hivi karibuni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |