Rais wa Kenya aahidi kuisadia DRC kurejesha utulivu wa kisiasa
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameeleza nia ya nchi yake kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kurejesha utulivu wa kisiasa.
Kenyatta alitoa ahadi hiyo wiki wii alipokuwa na mazungumzo na mwenazake wa DRC Felix Tshisekedi mjini Nairobi.
Amesisitiza kuwa Kenya imepata funzo zuri kutokana na vurugu za kisiasa zilizotokea huko nyuma, funzo ambalo Kenya iko tayari kuipatia DRC. Kenyatta amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakiwahifadhi wakimbizi wa Kongo, ambapo baadhi yao wamekuwa raia wa nchi hiyo na kwamba nchi hizo zina mambo mengi ya kubadilishana hususan urithi wa utamaduni.
Tshisikedi aliwasili Nairobi wiki hii ikiwa ni kituo chake cha pili kwenye ziara yake ya nchi tatu ambayo atamalizia nchini Jamhuri ya Congo na kufanya mazungumzo na rais Denis Sassou Nguesso.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |