• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 1-Juni 7)

    (GMT+08:00) 2019-06-07 16:43:34

    IGAD yazitaka pande husika za Sudan kujizuia

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD limetoa wito kwa pande zote husika za Sudan kujizuia zaidi.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, lina wasiwasi juu ya mapigano yanayopamba moto na kuzitaka pande husika za Sudan kufanya mazungumzo kwa nia ya kufikia mwafaka.

    Shirika hilo limesisitiza haja ya kulinda amani na utulivu nchini humo na kuwataka wadau wote wa Sudan kujizuia kwa kiasi kikubwa zaidi na kupunguza hali ya wasiwasi inayozidi kuwa mbaya.

    Shirika hilo pia limerejea tena ahadi yake ya kuendelea kushughulikia hali ya Sudan kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika, ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto za sasa.

    Viongozi wa waandamanaji nchini Sudan wamekataa wito wa mazungumzo uliotolewa na watawala wa kijeshi, wakitaka haki ipatikane dhidi ya wanajeshi waliohusika na mauaji ya raia zaidi ya 100 wiki hii.

    Wito wa jeshi unakuja ikiwa siku nne zimepita tangu litangaze kusitisha mazungumzo na waandamanaji pamoja na kufuta makubaliano yote yaliyokuwa yamefikiwa katika mazungumzo ya awali.

    Jumatatu ya wiki hii, vyombo vya usalama nchini humo vilitumia nguvu kubwa kuwaondoa maelfu ya raia waliokuwa wamepiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi, ambapo watu zaidi ya 100 wameuawa na wengine mamia kujeruhiwa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako