Umoja wa Mataifa watenga dola za kimarekani milioni 45 kuepuka hatari ya njaa katika Pembe ya Afrika
Umoja wa Mataifa umetenga dola za kimarekani milioni 45 ili kusaidia kuepuka hatari ya njaa katika eneo la Pembe ya Afrika.
Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja huo anayeshughulikia masuala ya kibinadamu Mark Lowcock amesema, fedha hizo kutoka Kituo Kikuu cha Mfuko wa Dharura (CERF) zitaongeza misaada ya dharura kwa watu walioathirika na ukame katika nchi za Somalia, Ethiopia na Kenya, ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na mvua chache zilizonyesha.
Amesema fedha hizo zitasaidia juhudi za serikali za nchi hizo tatu kupitia msaada kwa makundi mbalimbali ya watu hususan wale wenye ulemavu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |