Bw. Guterres asema Umoja wa Mataifa utaishiwa fedha mwezi Agosti mwaka huu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema fedha taslimu za umoja huo zingeisha mwezi Agosti mwaka huu, ambao utakopa fedha kutoka mfuko maalum wa Umoja huo.
Amesema katika miaka kadhaa iliyopita hali ya fedha ya Umoja wa Mataifa imekuwa mbaya siku hadi siku, hali ambayo inasababishwa na ongezeko la madeni ya nchi wanachama pamoja na sababu nyingine.
Hadi sasa madeni hayo yamefikia dola milioni 492 za kimarekani. Ameongeza kuwa kutolipa au kuahirisha kulipa mgao si sababu pekee ya upungufu wa fedha kwa umoja huo, suala la kimfumo kwenye mchakato wa kuweka mpango wa bajeti pia linasababisha hali hiyo.
Ametoa mapendekezo juu ya kutatua suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa mzunguko wa fedha taslimu, na kusimamia matumizi ya fedha kwa kuunga mkono utekelezaji wa bajeti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |