Somalia yaangazia uchaguzi wa amani licha ya changamoto za kisiasa
Maafisa wa ngazi ya juu wa Somalia wameeleza matumaini yao kwamba nchi itafanya uchaguzi wa amani na wa kuaminika mwaka 2020/2021 licha ya changamoto za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazoikabili nchi hiyo.
Maafisa waliohudhuria mkutano huo wa siku nne ulioandaliwa na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, wameyataka mashirika yote ya serikali yanayohusika na maandalizi ya uchaguzi kushirikiana pamoja ili kutimiza haki ya watu wazima wote kupiga kura.
Kwenye taarifa yake Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Somalia, Halima Ismail Ibrahim, amewataka wabunge waliohudhuria mkutano huo kutetea "mtu mmoja, kura mara moja" ndani ya seneti na bunge ili kuharakisha upitishaji wa sheria ya uchaguzi.
Tume hiyo ya uchaguzi imeanzisha mpango wa miaka mitano mwaka 2018 ili kusaidia kuongoza usimamizi na utawala wa nchi juu ya "mtu mmoja, kura mara moja" kwenye uchaguzi wa 2020/2021.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |