Boeing chapa 737 max bado ina matatizo yasema FAA
Wakaguzi nchini marekani wamegundua tatizo jipya katika ndege ya kampuni ya Boeing chapa 737 max ambalo huenda likachelewesha kurudi kuhudumu kwa ndege hiyo.
Utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) umesema umegundua "inayowezekana kuwa hatari" wakati wa majaribio, lakini haukfichua matokeo.
Ndege hiyo inayouzwa sana katika kampuni ya Boeing ilisitishwa mnamo Machi baada ya ajali mbili za ndege.
Kampuni hiyo inamarisha mfumo wa kutuwa kwa ndege hiyo, ambao unachunguzwa na maafisa wa uchunguzi wa ajali ya ndege.
Mwezi uliopita, FAA liliashiria kuridhia mabadiliko ya Boeing kwa ndege hiyo ya 737 Max ambayo yanaweza kuidhinishwa mwishoni mwa Juni.
Hilo lingeruhusu ndege hizo kufanyiwa majaribio mapema mwezi Julai.
Awali kulikuwa na matumaini kuwa ndege ya 737 Max itarudi angani wakati wamsimu wa joto, lakini mpangilio huo ulisukumwa mwishoni mwa mwaka huu.
FAA imesema kuwa wakati wa kufanyiwa majaribio kwa usukani wa rubani ambao mfumo wa kutua uliidhinishwa, ilichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kupata udhibiti wa ndege hiyo.
Vyanzo vingine vinasema tatizo linahusiana na nguvu ya kompyuta ya ndege hiyo na huenda haukuwa na uwezo wa kupokea maagizo kwa kasi inayohitajika.
Boeing imesema "Tunashirikiana kwa karibu na FAA kuirudisha kuhudumu ndege ya Max " na kwamba inaamini suluhu kwa mfumo huo utalitatua tatizo lililopo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |