Balozi wa China nchini Marekani asema China na Marekani zinapaswa kuweka mkakati sahihi juu ya uhusiano kati yao
Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema China na Marekani zinapaswa kuweka mkakati sahihi juu ya uhusiano kati yao katika siku za usoni, na kuweka mpango wazi wa maendeleo, ili kulinda na kuhimiza maslahi makuu ya wananchi wa nchi mbili na ya watu wa dunia nzima.
Akizungumzia suala la mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, Bw. Cui amesema watu wanaochochea mgogoro huo hawafahamu sera ya ujamaa wenye umaalum wa China, wala hawafahamu wazo la kutonufaishana na migogoro haziendani na wakati wa sasa, na uhusiano mpya kati ya nchi mbili ambao umekuwa jumuiya ya maslahi ya pamoja inayotegemeana.
Amesisitiza kuwa dunia ya hivi sasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita. China na Marekani zinapaswa kuongeza ufahamu, kuheshimiana, na kuimarisha ushirikiano na kufuata maoni ya raia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |