Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania watoa taarifa ya kiusalama
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa taarifa ya kiusalama katika maeneo yanayotembelewa na wageni katika jiji la kibiashara la nchi hiyo la Dar es salaam.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia tovuti ya Ubalozi huo, imeeleza kuwa kuna uvumi huenda mashambulizi hayo yakalenga mtaa wa kifahari wa Masaki, Hoteli ya Serena, Slipway na maeneo ya Msasani.
Hata hivyo, Ubalozi unasema hauna ushahidi wa kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini unatoa wito wa watu kuwa makini na kuepuka mikusanyiko wa watu wengi.
Mkuu wa jeshi la Polisi nchini humo Simon Sirro amesema anafahamu kuhusu uvumi huo na maafisa wa usalama wanazifanyia kazi.
Tanzania haijawahi kulengwa na visa vya mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni, isipokuwa mwaka 1998, wakati magaidi wa al-Qaeda waliposhambulia Ubalozi wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 11.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |