Malkia wa Uingereza aidhinisha kusitishwa kwa bunge
Malkia wa Uingereza Elizabeth ameidhinisha wiki hii kusitishwa kwa bunge kufuatia ombi la waziri mkuu mpya Boris Johnson.
Kufuatia kuidhinishwa kwa ombi hilo sasa bunge litavunjwa tu kwa siku kadhaa baada ya wabunge kurejea kazini mwezi Septemba - na wiki chache kabla ya muda wa mwisho ambao Uingereza ilipewa kuondoka katika muungano wa Ulaya
Malkia Elizabeth ameombwa na serikali kuvunja bunge siku chache tu baada ya wabunge kurejea kazini mwezi Septemba - kwenye Jumuiya ya Ulaya (EU) maarufu kama Brexit.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza Jeremy Corbyn amemwandikia barua Malkia Elizabeth kueleza kusikitishwa kwake na mpango wa waziri mkuu wa taifa hilo Boris Johnson wa kusitisha shughuli za bunge hadi Oktoba 14 baada ya malkia kuridhia ombi la serikali.
Ireland imekosoa uamuzi wa waziri mkuu Johnson wa kusimamisha bunge la nchi yake.
Baada ya Uingereza Jumatano kutangaza kusimamishwa kwa bunge, naibu waziri mkuu wa Ireland ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na biashara wa nchi hiyo Simon Coveney amesema, ni vigumu kuona kama kuna uwezekano mkubwa zaidi wa Brexit bila ya makubaliano.. Hatua ambayo inaaminiwa kuwa ni jaribio la Johnson kupunguza nafasi za wabunge kupitisha sheria za kuzuia Brexit bila ya makubaliano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |