Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na naibu mkuu wa kamati kuu ya chama tawala cha Korea Kaskazini
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na naibu mkuu wa kamati kuu ya Chama tawala Cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini, ambaye pia ni mjumbe wa ofisi ya kisiasa na mkuu wa idara ya kimataifa ya chama hicho Bw. Ri Su-yong mjini Pyongyang.
Bw. Wang amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kuwajibika, kulinda, kuimarisha na kuendeleza vizuri urafiki kati yao na kusukuma mbele ushirikiano wa sekta mbalimbali kati yao. Pia amesema, China na Korea Kaskazini zinapaswa kuongeza mawasiliano, maelewano na uaminifu ili kuungana mkono kulinda maslahi ya pamoja na haki zao.
Kwa upande wake, Bw. Ri amesema, Korea Kaskazini inapenda kushirikiana na China kuongeza mawasiliano na kusukuma mbele ushirikiano halisi ili kuendeleza uhusiano wao upate maendeleo zaidi. Bw. Ri pia amesema, Korea Kaskazini inapongeza utimiaji wa miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na mafanikio makubwa yamambo ya kijamaa ya China. Korea Kaskazini itaendelea kuunga mkono maslahi makuu na hatua zikatazochukuliwa na China katika masuala ya Hong Kong na Taiwan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |