Wabunge Uingereza wambana waziri mkuu
Waziri Mkuu wa Uingereza amepata pigo mara mbili, baada ya wabunge kukataa pendekezo lake la kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini pia, kukataa mswada wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.
Aidha, wabunge walio wengi, waliunga mkono pendekezo la nchi hiyo kupata kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na mkataba hata iwapo hili litafanyika baada ya Oktoiba 31, siku ya mwisho kujiondoa.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Boris Johnson akijibu maswali ya wabunge, alimkosea kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn kwa kuwapotosha raia wa Uingereza, kuhusu suala hili.
Amemtaka kiongozi wa upinzani athibitishe kuwa, iwapo muswada wake utapitishwa,awarahusu wananchi wawe na uamuzi kwa kuwa na uchaguzi mkuu tarehe 15 mwezi Oktoba.
Hata hivyo, wabunge wengi wakiongozwa na wale wa upinzani wanasema watakubali tu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu iwapo mkataba utapatikana.
Wabunge hao walikataa pia hoja ya Johnson ya kuiruhusu Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano mwezi ujao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |