Watu sita wafariki kwenye mafuriko katika hifadhi ya hells gate kenya
Watu sita wamethibitishwa kufariki katika Hifadhi ya Kitaifa ya Hell's Gate nchini Kenya baada ya kusobwa na maji ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa siku ya Jumapili.
Shirika la wanyamapori la Kenya KWS, limefunga hifadhi ya kitaifa ya Hell's Gate kufuatia mkasa huo.
Waliosombwa na mafuriko walikuwa watalii sita raia wa Kenya na mtu mmoja raia wa kigeni.
Watu hao walikuwa miongoni mwa kundi la watu 12 waliokuwa wanazuru hifadhi ya Hells Gate, karibu kilomita 100 Kaskazini magharibi mwa Jiji kuu la Nairobi.
yanayopita kati kati ya milima na ambayo husababisha mafuriko.
Eneo hilo linasifika kwa mandhari yake ya kupendeza ambayo pia imeangaziwa katika filamu ya The Lion King.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |