Serikali ya Malawi yawaondoa raia wake waliopoteza makazi kutokana na vurugu Afrika Kusini
Serikali ya Malawi imetangaza kuwa imekodi mabasi mawili ya kuwasafirisha raia wake waliopoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.
Katibu wa wizara ya kushughulikia majanga wa Malawi Bw. Wilson Moleni amesema mabasi hayo yaliondoka Johannesburg jumanne jioni na kutarajiwa kufika Malawi. Amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya ubalozi wa Malawi nchini Afrika Kusini kutoa taarifa kuwa wamalawi 113 nchini Afrika Kusini wamepoteza makazi. Kwa sasa watu hao wamepewa hifadhi katika mji wa Katlehong mashariki mwa Johannesburg. Kati ya hao, 76 wameeleza utayari wa kurudi nyumbani kwa hiari.
Wakifika nyumbani watu hao watapewa hifadhi ya muda mjini Blantyre kabla ya kurudi ma
Wakati huo huo Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais wa Afrika Kusini Bw. Jeffrey Radebe amesema Afrika Kusini imeiomba msamaha Ghana kufuatia mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni yaliyotokea nchini humo, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu kutoka nchi mbalimbali za Afrika, na biashara zao kuporwa.
Bw. Radebe amewasilisha maoni ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwenye mkutano kati yake na Rais Nana Akufo wa Ghana mjini Accra. Pia amesema Rais Ramaphosa ameamua kuahirisha kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa ili kushughulikia jambo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |