• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 14-Septemba 20)

    (GMT+08:00) 2019-09-20 18:23:34

    Boris Johnson asubiri hukumu yake kwa kusitisha bunge, huku Jean-Claude Junker akisema makubaliano ya Brexit yanawezekana

    Kesi ya kuamua kama Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amekwenda kinyume cha sheria wakati alipositisha bunge la nchi hiyo inakaribia huko London.

    Lakini Johnson atalazimika kusubiri hadi mwanzoni mwa wiki ijayo kusikiliza hukumu ya Mahakama ya Juu ya Uingereza. Katika hatua ya kupambana na Johnson, rais wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Junker amesema makubaliano ya Brexit yanawezekana hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba. Baada ya kutolewa tangazo hilo, paundi ya Uingereza imepanda kwa kiwango cha juu katika miezi kadhaa dhidi ya dola ya Marekani.

    Kwa siku tatu, wanasheria wa juu wanaowakilisha pande zote mbili wamekuwa wakitafuta njia ya kuhakikisha wanashinda juu ya kesi hiyo. Nao wataalamu wa sheria wanaoangalia sakata la kesi hiyo wamegawanyika juu ya matokeo yatakavyokuwa.

    Awali Johnson alikutana na mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker Jumatatu huko Luxembourg, ambapo amesisitiza kuwa nchi yake itajitoa kwenye Umoja wa Ulaya Oktoba 31.

    Akihojiwa na wanahabari wa Uingereza baada ya mkutano huo, Bw. Johnson amesema juhudi zimefanywa kwenye mazungumzo katika kutafuta mpango mbadala wa sera ya awali ya kuhakikisha mpaka wa Ireland unakuwa wazi kama ilivyokuwa sasa baada ya Brexit (Irish backstop), ili kuepusha uwekaji wa mpaka halisi wa kuzuia watu na mizigo kusafiri kwa uhuru katika kisiwa cha Ireland.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako