• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 19-Oktoba 25)

    (GMT+08:00) 2019-10-25 20:59:57

    Mahakama nchini Bangladesh yatoa hukumu ya kifo kwa watu 16 waliomuua mwanafunzi kwa kumchoma moto.

    Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 waliomchoma moto hadi kufa mwanafunzi kwa kuripoti kuwa mwalimu mkuu amenyanyasa kingono.

    Nusrat Jahan Rafi, 19, alifariki mwezi Aprili katika mji wa Feni, uliopo kilo mita 160 nje ya mji mkuu wa Dhaka.

    Mwalimu mkuu aliyetuhumiwa na Nusrat kwa unyanyasaji na wanafunzi wawili wa kike ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.

    Kifo chake kilishangaza nchi nzima na kusababisha msururu wa maandamano kushinikiza Nusrat apate haki.

    Kesi hiyo ni ya kwanza kuamuliwa haraka nchini ikilinganishwa na nyingine kama hizo ambazo huchukua miaka kadhaa kabla ya kuamuliwa. Mwendesha mashtaka Hafez Ahmed aliwaambia wanahabari kuwa "wauaji sharti wachukuliwe hatua Bangladesh".

    Uchunguzi wa mauaji ya Nusrat ulionesha njama ya kutaka kumnyamazisha ambayo pia ilihusisha wanafunzi katika darasa lake pamoja na wanaume walio na ushawishi mkubwa katika jamii.

    Walimu watatu wakiwemo mwalimu mkuu, Siraj Ud Doula, ambaye polisi inasema alitoa amri ya kuuwa kwa mwanafunzi huyo kutoka jela, walipatikana na hatia ya mauaji siku ya Alhamisi.

    Wengine wawili waliopatikana na hatia ni Ruhul Amin na Maksud Alam, kiongozi wa chama tawala cha Awami League party.

    Maofisa kadhaa wa polisi pia walipatikana na hatia ya kushirikiana na wale waliokamatwa kueneza taarifa za uwongo kwamba Nusrat alijitoa uhai.

    Vyombo vya habari vimeripoti kuwa familia ya Nusrat, ambayo iliunga mkono hatua yake kwenda polisi mwezi machi, imepewa ulinzi.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako