Tembo 55 wafa kutokana na ukame Zimbabwe
Tembo 55 wamekufa njaa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange, nchini Zimbabwe kutokana na ukame mkali uliokithiri kwa zaidi ya miezi miwili.
Msemaji wa mbuga hiyo Tinashe Farawo, anasema alisema Tembo wanakufa kutokana na ukame na hilo ni tatizo kubwa.
Ukame umepunguza kwa kiwango kikubwa viwango vya mimea nchini Zimbabwe.
Theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wakati mgogoro wa kiuchumi ukiendelea nchini humo.
Mwezi Agosti, ripoti ya Shirika la Chakula Duniani ilisema kuwa watu milioni mbili wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
Baadhi ya tembo walipatikana katika eneo la mita 50 (yadi) ya maji -kuashiria kuwa walitembea mwendo mrefu bila maji na hatimaye kufa muda mfupi kabla ya kuyafikia.
Tembo hao wamesababisha "uharibifu mkubwa" wa mimea katika mbuga ya Hwange, Bw. Farawo alisema.
Mbuga hiyo inawahifadhi karibu tembo 15,000 lakini kwa sasa kuna zaidi ya tembo 50,000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |