• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 16-Novemba 22)

    (GMT+08:00) 2019-11-22 21:11:20
    Netanyahu akataa kuondoka madarakani

    Waziri mkuu Benjamini Netanyahu wan chi ya Israel amedinda kuondoka madarakani baada ya kushtakiwa na tuhuma za kutoa rushwa , kufanya udanganyifu na kuvunja imani ya raia waliomchagua kuhusiana na kesi tatu tofauti.

    Hata hivyo Netanyahu ametaja mashtaka hayo kuwa jaribio la mapinduzi dhidi yake. Amesisitiza kuwa hatokubali uongo kushamiri. Bwana Netanyahu alidaiwa kukubali kuchukua zawadi kutoka kwa wafanyabiashara matajiri na kutoa hongo ili kuweza kuwa katika vyombo vya habari mara kwa mara. Katika hotuba ya dakika 15 , Netanyahu ameilaani idara ya mahakama , maafisa wa polisi na wengine kwa kupanga njama dhidi yake wakiwa na nia yenye madai ya msukumo wa kisiasa. Awali mwanasheria mkuu Avichai Mandelblit alisema kwamba alitoa uamuzi huo kwa 'moyo mzito' lakini akasema imeonyesha kwamba hakuna asiyeweza kushtakiwa nchini Israel. Tangazo hilo linajiri huku kukiwa na mkwamo wa kisiasa nchini humo kufuatia chaguzi mbili kuu ambazo hazikutamatishwa mwezi Aprili na Septemba. Jumatano wiki hii, mpinzani wa Bwana Netanyahu Benny Gantz alisema kwamba ameshindwa kubuni serikali ya muungano na walio wengi bungeni.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako