• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 16-Novemba 22)

    (GMT+08:00) 2019-11-22 21:11:20

    Watoto 5000 wafariki kutokana na ugonjwa wa ukambi DRC

    Ugonjwa wa ukambi unasemekana kuwaua takriban watoto 5000 katika nchi ya Jamhuri ya KidemokrasIa ya Congo mwaka huu. Kulingana na mamlaka husika ugonjwa huo ulisambaa hadi mikoa yote nchini humo. Inadaiwa mwaka huu pekee, watoto 250,000 wameambukizwa ugonjwa huo.

    Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa huo ndio janga linalosambaa kwa kasi mno.

    Taarifa zinasema ugonjwa huo wa ukambi nchini DR Congo umeua idadi ilio mara mbili ya wagonjwa waliofariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika kipindi cha miezi 15 iliopita. Hivi sasa serikali ya DRC kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO imezindua chanjo ya dharura mwezi Septemba inayowalenga watoto 800,000.

    Lakini miundo msingi mibaya, mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, mbali na ukosefu wa tiba za mara kwa mara zimekwamisha juhudi za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

    Watoto milioni 4 tayari wamepewa chanjo, lakini wataalam wameonya kwamba idadi hiyo ni chini ya nusu ya jumla ya watoto nchini humo na kwamba chanjo zilizopo hazitoshi.

    Wengi ya wale walioathirika na ugonjwa huo ni watoto wachanga.

    Mwanamke mmoja nchini Tanzania ameshangaza watu nchini humo pale alipomchinja mwanae wa miaka minne na kula baadhi ya viungo vyake huku vingine vikipotelea porini. Tukio hilo limechukuliwa na wengi kuwa la kushangaza na lilitokea katika mkoa wa Njombe Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania baada ya

    Tukio hilo linadaiwa kufanyika kugundulika baada ya mume wake kurudi nyumbani kutoka shambani siku ya jumapili saa 12 jioni.

    Mume wake aliporejea nyumbani alimkuta mtoto mmoja tu nyumbani na alipomuuliza mke wake mtoto mwingine yuko wapi? akajibiwa kuwa anatakiwa kwenda kulipa mahari akiwa anamaanisha kupeleka ng'ombe na mbuzi kwao.

    Vilevile mke alidai kuwa alimwambia mume wake muda mrefu kumpeleka kwa wazazi wake lakini hakutaka kwenda kwa hiyo hana mamlaka ya kumuuliza mtoto yuko wapi.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako