Watu 7,000 wahanga wa mabomu ya ardhini
Ripoti iliyotolewa hivi majuzi inaonesha kuwa mwaka jana peke yake zaidi ya watu 7,000 walikuwa wahanga wa mabomu ya kutegwa ardhini. Pamoja na marufuku iliyowekwa zaidi ya miaka 20 iliyopita dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini, vifo vinavyotokana na mabomu hayo bado vinaendelea kutoke. Kwa mujibu wa shirika la kutoa misaada la Handicap International la mjini Munich nchini Ujerumani, mwaka 2018 kulikuwa na jumla ya matukio 6,897 ya kulipuka kwa mabomu ya kutegwa ardhini, ambapo mabomu hayo yalisababisha majeraha na vifo, hususan katika nchi za Afghanistan, Libya, Nigeria na Syria. Mwaka 1997 mjini Ottawa nchini Canada kulipitishwa hatua ya kupiga marufuku mabomu yote ya kutegwa ardhini. Nchi zilizosaini makubaliano hayo zinatarajiwa kukutana mjini Oslo, Norway, kwa ajili ya mkutano wa kutathimini hatua hiyo ya marufuku.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |