Waasi katika jimbo la Ituri wamevishambulia vituo viwili vya matibabu ya Ebola vinavyoendeshwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), katika uvamizi uliofanyika usiku wa kuamkia Alhamisi na kuwauwa wahudumu watatu.
Taarifa zinasema kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni wafanyakazi wa WHO na kwamba watu wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa mashuhuda, waasi waliwazidi nguvu polisi kwenye vituo hivyo vilivyopo katika maeneo ya Mangina na machimbo ya Biakato.
Magari manne yamechomwa moto pamoja na majengo kadhaa yameteketezwa.
Maafisa wakuu wa shirika hilo akiwemo Mkurugenzi Mkuu Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus wamelaani shambulio hilo lililosababisha vifo na majeruhi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |