• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 23-Novemba 29)

    (GMT+08:00) 2019-11-29 19:17:46

    Ripoti ya BBI yazinduliwa rasmi nchini Kenya

    Kamati ya BBI ilizindua rasmi ripoti yake mbele ya viongozi wa kisiasa nchini Kenya katika ukumbi wa Bomas. Kwenye mapendekezo ya BBI, rais aliyechaguliwa na wengi atahitaji washirika wengi bungeni kuhakikisha kwamba kuna upitishwaji wa haraka wa miswada mbali na kuidhinishwa maswala muhimu ya biashara za serikali iwapo mapendekezo ya BBI yatakubalika.

    Kamati ya BBI pia inapendekeza kwamba rais atamchagua waziri mkuu, mawaziri na manaibu wao kutoka kwa wabunge waliochaguliwa kinyume na serikali ya sasa ilivyo ambapo mawaziri wanachaguliwa kutoka nje.

    Fursa pia imetolewa kwa rais kuwachagua watu binafsi ambao sio wabunge lakini ambao watakauwa wabunge wa zamani, ikimaanisha kwamba wataruhusiwa bungeni lakini hawatakuwa na uwezo wa kupiga kura ili kuidhinisha miswada. waziri mkuu atachaguliwa miongoni mwa wabunge na lazima atoke kutoka chama chenye wanachama wengi katika bunge ama mtu aliye na ufuasi mkubwa iwapo kutakuwa na serikali ya muungano.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako