Rwanda na Tanzania zafanya mazungumzo ya kujenga reli ya SGR ya pamoja
Rais John Magufuli amesema serikali za Tanzania na Rwanda zinafanya mawasiliano ya mwisho ya mazungumzo kujenga reli ya kasi SGR kutoka bandari kavu ya Isaka nchiniTanzania hadi Rwanda.
Rais Magufuli amesema hayo akihutubia umma kwenye bandari kavu ya Isaka iliyoko sehemu ya Kahama akiwa njiani kuelekea Shinyanga, huku akisema kuwa reli hiyo ya SGR pia itahudumia nchi zisizo na bahari zikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Pia amesema rais Paul Kagame amekubali kimsingi kutekeleza mradi huo wa pamoja. Upembuzi kuhusu uwezekano wa kujengwa kwa reli ya SGR inayounganisha Tanzania na Rwanda umefanyika, na nchi hizo mbili zinatafuta wafadhili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |