Iran yatakiwa kutotengeneza silaha za masafa marefu
Iran imetakiwa kutotengeneza silaza za masafa marefu zilizo na muundo wa kubeba nyuklia, ikiwemo kurusha makombora kupitia teknolojia hiyo ya makombora ya masafa marefu. Hayo ni kwa mujibu wa azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa 2231 linatoa wito kwa Iran kutotengeneza silaha hizo.
Iran imesisitiza kuwa mpango wake wa Kinyuklia ni wa amani na kukana madai kwamba mpango wake wa kutengeneza makombora ya masafa marefu unakiuka azimio hilo. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani inasema kwamba Iran ilifanyia majaribio silaha yake aina ya Shahab 3 ilioshikana na gari ambalo linaweza kusukuma silaha ya kinyuklia.
Hata hivyo waziri wa masuala ya kigeni Mohammed Javad Zarrif amesema barua hiyo ilikuwa ya uongo iliyoandikwa na mataifa hayo ya Ulaya ili kuziba uzembe wao wa kushindwa kuafikia makubaliano ya mpango wa kinyuklia wa Iran. Azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa 2231 linatoa wito kwa Iran kutotengeneza silaza za masafa marefu zilizo na muundo wa kubeba nyuklia, ikiwemo kurusha makombora kupitia teknolojia hiyo ya makombora ya masafa marefu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |