Ufaransa yashuhudia mgomo mkubwa wa wafanya kazi
Ufaranfa umeshuhudia mgomo mkubwa wa wafanyakazi ulioitishwa na chama cha wafanya kazi nchini humo. Mgomo huo wa kitaifa uliathiri shule na usafiri wa umma nchini Ufaransa.
Wafanyakazi walikasirishwa na mpango wa kuwalazimisha kustaafu kuchelewa ama malipo yao ya uzeeni yapunguzwe.
Maafisa wa polisi, mawakili, wafanyakazi wa hospitali na viwanja vya ndege wameungana na wafanyakazi wa shule na sekta ya usafiri wa umma katika mgomo wa kitaifa ambao huenda ukajumuisha mamilioni ya watu.
Maandamano hayo makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi yaliidhinishwa na chama cha wafanyakazi ambacho hakijafurahishwa na mipango ya rais Macron ya kutaka kuanzisha mfumo wa malipo ya uzeeni ambapo kila siku moja iliyofanyiwa kazi inapata alama kwaajili ya mapato ya pensheni ya siku za usoni.
Mamlaka imekuwa ikijaribu kuweka mipango ya kuanzisha mfumo huo.
Gazeti la Ufaransa la Le Monde, lilinukuliwa likisema "Maandamano hayo ni mtihani mkubwa kwa Macron".
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |