AU yataka mizigo wa ugonjwa wa ukimwi kupunguzwa
Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat wiki hii ametoa wito wa kuwepo kwa juhudi za makusudi kupunguza mzigo wa ugonjwa wa UKIMWI kwa watu wazima walioko kwenye makundi yaliyo hatarini, hasa wakimbizi, watu wanaorudi makwao na wakimbizi wa ndani.
Akiongea jana wakati wa maadhimisho ya siku ya kupambana na UKIMWI duniani, Bw. Mahamat amesema makundi hayo yako hatarini zaidi, kama ilivyo kwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na miaka 19, ambao wako kwenye hatari kubwa ya maambukizi mapya. Bw. Mahamat pia amesema kuna haja ya haraka na kuweka mkazo kwenye kukabiliana na uhusiano kati ya maambukizi ya virusi vya UKIWMI na mabavu ya kijinsia, hasa kwenye mazingira ya kibinadamu na kwenye migogoro.
Siku hiyo imeadhimishwa wakati kukiwa na habari za kuridhisha kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, licha ya changamoto zinazoendelea kuwepo katika nchi mbalimbali. Nchini Afrika Kusini, Naibu Rais wa nchi hiyo Bw. David Mabuza amesema Afrika Kusini sasa inauchukulia ugonjwa wa UKIMWI kuwa ni hatari ya afya kwa umma, na inapanga kutokomeza ugonjwa huo kabla ya mwaka 2030. Hata hivyo amesema safari ya kuhakikisha hakuna maambukizi mapya, hakuna unyanyapaa na hakuna vifo imekuwa ndefu na ngumu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |