• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 4-Januari 10)

    (GMT+08:00) 2020-01-10 19:15:46

    Bunge la Kongresi la Marekani lapiga kura kuzuia vita dhidi ya Iran

    Alhamisi iliyopita Bunge la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha azimio linalolenga kumzuia Rais Donald Trump kupigana vita na Iran. Bunge hilo ambalo linafahamika pia kama Kongresi limepitisha azimio hilo kwa kura 224 dhidi ya 194.

    Hata hivyo azimio hilo lililopitishwa na Kongresi ambayo ina wawakilishi wengi zaidi wa Democrats litakutana na wakati mgumu kwenye bunge la Seneti linalotawaliwa na wawakilishi wengi zaidi kutoka chama cha rais Trump cha Republicans.

    Azimio hilo linalenga kuipa Kongresi nguvu ya kutoa kibali cha shambulio lolote dhidi ya Iran, isipokuwa pale tu patakapokuwa na shambulio la ghafla dhidi ya Marekani.

    Kwa sasa hakuna upande kati ya Iran na Marekani ambao umetamka kuwa utaendelea na mashambulizi.

    Jumatano wiki hii, Iran ilishambulia kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq baada ya Marekani kumuua Jenerali wa Iran Qasem Soleimani wiki iliyopita.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako