Ndege ya Ukraine yaanguka Iran na kuua watu 176
Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria zaidi ya 170 ilianguka Iran tarehe 8 Januari na kuua watu wote waliokuwa ndani.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.
Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.
Serikali ya Ukraine imesema kuwa inafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo.
Abiria wapatao 168 na wafanyakazi 9 wa ndege hiyo wamethibitishwa kuwepo kwenye ndege hiyo, Waziri mkuu Oleksiy Honcharuk alisema.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |