Maadhimisho ya siku ya ukeketaji dhidi ya wanawake Duniani
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) pamoja na wadau wake alhamisi,tarehe 6 wameadhimisha siku ya kupinga ukeketaji Duniani na kupinga vikali ukeketaji dhidi ya mwanamke na watoto.
Akizungumza wakati maadhimisho hayo Fatima Kiluria alisema kuwa kampeni hiyo ilifanyika alhamisi kwa kuwa ni Siku ya kupinga ukeketaji Duniani.
Baada ya ufunguzi huo walipata nafasi ya kuongea wanaharakati mbalimbali ambao wengine ni waathirika wa moja kwa moja wa suala la Ukeketa. Mmoja ni Mama au Ngariba ambaye alikuwa anakeketa watoto na ameongeza alikuwa na uwezo wa kukeketa watoto 100 kwa siku ingawa kwa sasa ameacha na ameanza kufanya harakati za kupinga tatizo hili kwa jamii.
Mbali na hilo pia ameongeza vitendo vya ukeketaji hupoteza watoto wadogo wengi sana kwani wengi hutokwa na damu nyingi na pale wanapopoteza maisha hutupwa porini ili waliwe na wanyama wakali kwani wakizikwa jamii kwa tamaduni zao huo kama analeta balaa.
Akitolea mfano mkoa wa mara amesema kuwa watoto wanapokeketwa hufungwa porini huku wakinyeshewa nvua hadi pale watakapopona na mara nyingi hupoteza maisha kwani hukutana na mazingira tofauti maporini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |