Waziri mkuu Li Keqiang aongoza mkutano wa kikundi cha uongozi cha kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye pia ni kiongozi wa kikundi cha uongozi cha kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona, Alhamisi aliongoza mkutano wa kikundi hicho.
Mkutano huo umeagiza idara zote husika zifuate mikakati na maamuzi yaliyotolewa na kikundi hicho cha uongozi, na kuchukua hatua madhubuti kuimarisha kazi za kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona kote nchini kwa mujibu wa sheria, sayansi na kwa utaratibu.
Mkutano huo umeainisha kuwa mkoa wa Hubei, hasa mji wa Wuhan bado ni kipaumbele katika cha kazi za kudhibiti mlipuko wa virusi hivyo, na pia umezitaka idara husika ziendelee kuinua kiwango cha kuwapokea na kuwatibu wagonjwa, kutuma madaktari na vifaa zaidi mkoani Hubei na kuhakikisha uzalishaji na ugavi wa vifaa muhimu vya kimatibabu vinavyohitajika katika vita dhidi ya virusi vya korona.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |