Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Serikali zenye uwezo mkubwa wa kipato kuchangia dola bilioni 6.7 kusaidia mataifa masikini
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Serikali zenye uwezo mkubwa wa kipato, kampuni na matajiri duniani kuchangia dola bilioni 6.7 kusaidia mataifa masikini kupambana na virusi vya corona.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kutoa wito mpya kwa ulimwengu kuchangia fedha kuzisaidia nchi masikini, mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amesema mataifa yenye uwezo duni yanakabiliwa na kitisho maradufu cha athari za virusi vya corona.
Lockcock ameonya kuwa kushindwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha janga la njaa, machafuko na mizozo zaidi.
Lowcock amesema ugonjwa wa COVID-19 tayari umeathiri kila nchi na kila mtu duniani na kilele cha janga hilo kinatarajiwa kuleta mtikisiko kwa mataifa masikini kwa muda wa miezi mitatu hadi sita inayokuja.
Amesema ombi la awali la Umoja wa Mataifa la dola bilioni 2 limeongezeka kwa sababu ushahidi unaonesha watu wengi wanapoteza kipato, hakuna nafasi za kazi, bei za vyakula zimepanda na watoto wanakosa chanjo na matibabu muhimu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |