CHUO cha Jomo Kenyatta ( JKUAT kimeonyesha ubunifu wa kuunda mitambo miwili tofauti aina ya sola.
CHUO cha Jomo Kenyatta ( JKUAT), eneo la Juja, Kaunti ya Kiambu, kimeonyesha ubunifu wa kuunda mitambo miwili tofauti aina ya sola.
Mmojawapo wa mitambo hiyo ni aina ya sola inayotumika kidijitali ambayo ikiunganishwa kwa mitambo ya kuleta hewa, pia inakadiria aina ya viini vya Covid-19.
Mtambo mwingine ni wa kunawa mikono kupitia umeme.
Naibu Chansela wa JKUAT Prof Victoria Ngumi amesema ubunifu huo wa kipekee ni kazi ya wanafunzi wa chuo hicho wanaobobea katika taaluma za teknolojia na uhandisi na wanaozama kufanya utafiti wa hali ya juu.
Mmoja wa wanafunzi hao katika ubunifu huo, Bw Karanja Kabini, amesema mitambo hiyo ni za kipekee na kulingana na jinsi ilivyoundwa, inaendeshwa kwa wiki mbili mfululizo bila kufanyiwa marekebisho yoyote ya kimitambo.
Prof Ngumu, amesema wanafunzi hao wa kitengo cha uhandisi wana uwezo wa kuunda mitambo ya kusaidia wagonjwa kupumua – ventilators – kwa wiki moja.
HAKUNA kuingia wala kutoka mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi na Mji wa Kale ulioko Mombasa usiku na mchana kwa muda wa siku 15 zijazo
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |