Wakenya waliorudi nyumbani watalazimika kwenda karantini kwa siku 14.
Ubalozi wa Kenya huko Beijing pia umepanga na Kenya Airways kuwarudisha raia walioko nchini China nyumbani.
Hata hivyo wale wanaosafiri watalazimika kutoa cheti cha kibali kutoka kwa kituo cha afya kinachothibitishwa kuwa hawana virusi vya corona.
Katibu Mkuu wa Mambo ya nje Balozi Macharia Kamau alitangaza mipango ya kurudisha Wakenya wapatao 500 walioko nchini China, India na Uingereza kwa gharama zao wenyewe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |