Bunge la umma la China lapitisha azimio la kujenga mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa mkoa wa Hong Kong
Bunge la Umma la China leo limepitisha azimio kuhusu kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa Mkoa wenye Utawala Maalum wa Hong Kong, na kuamua kutekeleza azimio hilo tangu wakati lilipopitishwa.
Azimio hilo limeeleza kuwa, bunge hilo limefanya uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Watu wa China ili kulinda mamlaka, usalama, na maslahi ya maendeleo ya taifa, kushikilia na kuboresha sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", kulinda utulivu na ustawi wa kudumu wa Hong Kong, na kuhakikisha haki halali za wakazi wa Hong Kong.
Azimio hilo limeweka bayana kwamba China inashikilia kithabiti na kutekeleza kwa pande zote na usahihi mwongozo wa "Nchi Moja, Mifumo Miwili", "Watu wa Hong Kong waitawala Hong Kong", huku likisisitiza kuwa hatua za lazima zitachukuliwa kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa Hong Kong, kuzuia, kusimamisha na kuadhibu vitendo na shughuli zinazoharibu usalama wa taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |