Hotuba ya kwanza ya Rais mteule Burundi, Ndayishimiye amtaja Nkurunziza na Jumuiya ya kimataifa "Ushindi wangu ni wa raia wote"
Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi, Evariste Ndayishimiye alitangazwa mshindi jumatatu kwenye kinyang'anyiro cha urais nchini humo.
Ndayishimiye alitangazwa kushinda baada ya kupata asilimia 68.72 ya kura zilizopigwa. Tume ya uchaguzi nchini Burundi ambayo imetangaza matokeo hayo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini humo, imesema Agathon Rwasa wa chama cha National Freedom Council (CNL) ambaye ndiye mshindani mkuu wa Ndayishimiye amepata asilimia 24.19 ya kur
Evariste Ndayishimiye alisema ushindi wake ni wa raia wote waliomchagua na wale ambao hawakumchagua.
Akihutubia baada ya kutangazwa mshindi Ndayishimiye amesema ushindi wake ni wa raia wote waliomchagua na wale ambao hawakumchagua.
Hivyo hakuna sababu ya wafuasi wa chama kimoja kuwabugudhi wengine. Pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono hatua iliyofikiwa nchini humo.
Kiongozi huyo wa chama cha CNDD-FDD aliyeibuka mshindi uchaguzi wa Mei 20 ameongeza kusema kuwa uchaguzi huu umedhihirisha kukuwa kwa umahiri wa kisiasa wa Burundi. Ndayishimiye ameahidi kuwasikiliza raia wote Burundi bila ubaguzi.
"Tumejipa hadhi mbele ya Warundi na dunia, kwa kuionesha kuwa tulipofikia hatufundishwi tena demokrasia bali tunaweza kuwafundisha wengine. Hivyo ninaahidi kuwa nitawasikiliza wananchi wote bila ubaguzi ili maoni yao yaweze kulijenga taifa. Hivyo naitaka jumuia ya kimataifa kuiunga mkono hatua hii ya kupendeza tuliyoifikia". amesema Ndayishimiye
Pia Ndayishimiye amemshukuru mtangulizi wake Rais Pierre Nkurunziza kwa hatua yake ya kuridhia alivyoridhia kuanzisha mchakato huu wa uchaguzi. Ndayishimiye amewataka wakimbizi kurudi nyumbani kuchagina katika ujenzi wa taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |