• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 24-Oktoba 30)

    (GMT+08:00) 2020-10-30 20:54:24

    SHULE HAZITAFUNGWA LICHA YA CORONA KUSAMBAA ZAIDI KENYA

    Serikali imesisitiza kuwa shule hazitafungwa licha ya virusi vya corona kuzidi kuongezeka katika siku za hivi karibuni, ambapo walimu 33 wameambukizwa virusi hivyo.

    Katibu wa Wizara ya Elimu Belio Kipsang' jana aliwaambia wabunge kwamba wafanyakazi wanne wa shule pia wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

    Dkt Kipsang' alieleza kuwa jumla ya shule 35 kote nchini zimenakili visa vya ugonjwa huo. Hata hivyo, alitupilia mbali uwezekano wa shule kufungwa kutokana na hali hiyo.

    Mnamo Jumapili Waziri wa Elimu George Magoha pia alisisitiza kuwa shule hazitafungwa licha ya ripoti kuhusu maambukizi ya Covid-19.

    Baadhi ya washikadau wamekuwa wakihimiza shule kufungwa.Wakati huo huo, Prof Magoha jana alisema agizo la serikali kwamba shule zifunguliwe kwa wanafunzi wa Darasa la Nne, Nane, na Kidato na Nne linafaa kutekelezwa na shule zote.

    Shule zinazotumia mtaala wa kimataifa zilikuwa zimepanga kuruhusu wanafunzi wote kurejea shuleni kuanzia Jumatatu wiki hii, lakini mpango huo ukabatilishwa wakati ilipobainika kwamba maambukizi ya virusi vya corona yanapanda kwa kasi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako