• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 24-Oktoba 30)

    (GMT+08:00) 2020-10-30 20:54:24
    ULAYA YAANZA KUWASIHI WATU KUSALIA MANYUMBANI KUTOKANA NA WIMBI LA PILI YA CORONA.

    Hisa katika masoko makubwa duniani zimeanguka kufuatia ripoti kwamba nchi zenye uchumi mkubwa duniani zimerudisha masharti ya watu kusalia nyumbani kama ilivyokuwa awali na kupelekea uchumi wa dunia kudorora.

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa ujerumani Angela Merkel wameziamuru nchi zao kurejesha kwa tena amri ya watu kusalia nyumbani kwao kudhibithi wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona yanayotishia nchi za ulaya.

    Hisa katika masoko makubwa duniani zimeanguka kufuatia ripoti kwamba nchi zenye uchumi mkubwa duniani zimerudisha masharti ya watu kusalia nyumbani kama ilivyokuwa awali na kupelekea uchumi wa dunia kudorora.

    Macron amesema kwamba "virusi vya Corona vinasambaa kwa kasi sana kuliko ilivyotabiriwa na kwamba wamezidiwa na kasi ya virusi hivyo."

    Ameendelea kusema kwamba "virusi vya Corona vinaendelea kusababisha madhara makubwa na huenda hali ikawa mbaya zaidi ya ilivyokuwa wakati wa wimbi la kwanza."

    Serikali ya Ufaransa imewataka watu kusalia nyumbani na kuruhusiwa tu kutoka nje iwapo wanaenda kununua bidhaa muhimu, kutafuta huduma za afya, au kufanya mazoezi.

    Wafanyakazi pia wanaruhusiwa kwenda kazini iwapo mwajiri wao anaonelea kwamba lazima wafike kazini na kazi hiyo haiwezi kufanywa wakiwa nyumbani.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako