• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Je, New Zealand itakuwa kituo kinachounganisha Latin Amerika na China?

    Takwimu mpya zimeonesha kuwa mwezi wa Machi, thamani ya jumla ya mauzo ya bidhaa kwa nje ya New Zealand imefikia dola bilioni 3.76 za kimarekani na kuweka rekodi ya juu zaidi. Idara ya takwimu ya nchi hiyo imesema, rekodi hiyo inategemea ongezeko la mauzo ya bidhaa zake kwa China. Ukweli ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni China imeipita Australia na kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa New Zealand. Thamani ya biashara za pande mbili kati ya China na New Zealand imezidi dola bilioni 19.8 za kimarekani.

    • China inafungua mambo ya fedha kwa mpango wake mwenyewe
    Mwenyekiti wa Tume ya Kusimamia Benki na Bima nchini China Guo Shuqing amesema hivi karibuni China itatangaza hatua mpya 12 zinazolenga kufungua zaidi sekta ya benki na bima kwa nchi za nje.
    • "Ukanda mmoja, njia moja" Pendekezo muhimu kwa dunia iliyo wazi zaidi

    Mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la "ukanda mmoja, njia moja" umefungwa jana hapa Beijing, na baadaye taarifa ya pamoja kutolewa baada ya mkutano wa majadiliano wa viongozi.

    • Dhamira na malengo ya Ukanda Mmoja Njia Moja yatoa msukumo kwa mataifa yanayoendelea kuukumbatia mpango huo

    Mwaka 2017 iliashiria hatua ya kihistoria ya uhusiano wa China na ulimwengu. Aidha, mwaka huo ulikuwa wenye matukio mahsusi hasa kwa uhusiano kati ya China na Afrika. Utaratibu mpya wa dunia uliibuka.

    • Ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kuingia katika kipindi cha maendeleo ya sifa ya juu

    Mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utakaofanyika kwa siku tatu umefunguliwa leo hapa Beijing, na wajumbe 5,000 hivi kutoka nchi zaidi ya 150 na mashirika zaidi ya 90 ya kimataifa wamehudhuria mkutano huo. Baada ya maendeleo ya kasi ya miaka miwili, ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umekuwa jukwaa kubwa zaidi la kiuchumi na pendekezo la umma linalopendwa zaidi na pande nyingi lililotolewa na China kwa dunia nzima.

    • Idara ya safari ya anga ya juu ya China yatoa fursa ya ushirikiano kwa jumuiya ya kimataifa

    Leo ni siku ya nne ya safari za anga ya juu ya China, habari nyingi za kusisimua zimetolewa: China imetangaza maendeleo mapya ya utafiti wa kituo cha anga ya juu na imefanikiwa kurusha vyombo 12 vya safari za anga ya juu, chombo cha anga ya juu Tiangong-1 na maabara ya Tiangong-2, huku ikituma wanaanga 11 kwenye anga ya juu na kuwarejesha salama; satelaiti ya 44 ya Beidou hivi karibuni imerushwa katika anga ya juu na kuzindua uundaji wa mtandao wa satelaiti za Beidou kwa mwaka 2019; hasa katika operesheni ya uchunguzi wa mwezi ya Chang'e 6 itakayotekelezwa, na operesheni ya kurejesha sampuli kutoka kwenye sayari ndogo, China pia itatoa fursa ya ushirikiano kwa jumuiya ya kimataifa.

    • Jeshi la majini la China kuendelea kufanya juhudi kujenga jumuiya ya bahari yenye mustakabali wa pamoja
    Shughuli za maadhimisho ya miaka 70 ya jeshi la majini la China zimefanyika huko Qingdao,China Rais Xi Jinping wa China amekutana na viongozi wa ujumbe wa majeshi ya majini ya nchi mbalimbali, huku akikagua kundi la manowari na kundi la ndege la jeshi la majini la China, na kundi la manowari la majeshi ya majini ya nchi mbalimbali yanayoshiriki kwenye shughuli hizo. Rais Xi pia kwa mara ya kwanza ametoa pendekezo la kujenga jumuiya ya bahari yenye mustakabali wa pamoja, ambalo limeweka bayana mwelekeo wa maendeleo ya jeshi la majini la China, na kuhimiza mawasiliano kati ya China na nchi za nje kwenye bahari na ushirikiano katika sekta mbalimbali.
    • Rais Xi Jinping wa China aandika barua ya kujibu wanafunzi wa sekondari ya juu wa Marekani

    Kuhusu Rais Xi Jinping wa China kuandika barua kwa kujibu wanafunzi wa sekondari ya juu wa Marekani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amesema hii si mara ya kwanza kwa rais Xi kuandika barua kwa wanafunzi wa nchi za nje, ambayo inaonyesha kufuatilia kwake ushirikiano wa mawasiliano wa China na nchi za nje.

    • Uamuzi uliotolewa na WTO kwa ajili ya China hauashirii ushindi wa upande wowote

    Shirika la Biashara Duniani WTO tarehe 18 lilitoa uamuzi kuhusu ombi lililotolewa na Marekani mwezi Desemba mwaka 2016, la utatuzi wa mgogoro kuhusu usimamzi wa viwango vya ushuru kwa mazao ya ngano, mchele na mahindi ya China. Uamuzi huo unaona kuwa hatua ya China haiko wazi, na inakwenda kinyume na ahadi iliyotoa wakati wa kujiunga na WTO, lakini shirika hilo pia halikubaliani na ombi la Marekani kuitaka China kutangaza mpango wake wa viwango vya ushuru kwa bidhaa hizo.

    • China ni nchi inayodumisha utulivu wa biashara duniani

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonyesha kuwa thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje wa China katika robo ya kwanza ya mwaka huu ilifikia yuan trilioni 7.01, sawa na dola za kimarekani trilini 1.04, likiwa ni ongezeko la asilimia 3.7.Wakati mvutano wa biashara duniani unaongezeka, na kasi ya ongezeko la biashara duniani inapungua, matokeo iliyopata China katika biashara na nchi za nje katika kipindi hicho, hayakupatikana kwa urahisi, na kuonesha nguvu ya uhimili ya uchumi wa China, na nguvu kubwa iliyojifichika katika soko la China.

    • China kuendelea kuwa msukumo muhimu wa kuhimiza ongezeko la uchumi duniani
    Idara ya Takwimu ya China imesema, mwezi Machi faharisi ya bei za walaji ya China yaani CPI cha China kimepungua kwa asilimia 0.4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.3 kuliko mwaka jana wakati kama huu, huku kiashiria cha uzalishaji PPI kikiongezeka kwa asilimia 0.1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.4. Siku moja kabla ya hapo, Shirika la Fedha Duniani IMF lilipandisha makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka 2019 hadi asilimia 6.3, ambalo linaongezeka kwa asilimia 0.1 kuliko makadirio ya mwezi Oktoba. China imekuwa nchi pekee ambayo makadirio ya ongezeko la uchumi yamepandishwa kati ya makundi matano muhimu ya uchumi duniani.
    • Viongozi wa China na Ulaya wakubaliana kupanua maslahi ya pamoja na mafanikio ya kunufaishana
    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameanza ziara yake katika nchi za Ulaya, ikiwa ni baada ya rais Xi Jinping kufanya ziara ya kwanza katika nchi tatu za Ulaya mwaka huu, hatua ambayo imeonesha umuhimu wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ulaya.
    • Marekani yaendelea kuingilia kati mambo ya Mashariki ya Kati
    • China yajiunga na kigezo cha ujumla cha Barclays cha Bloomberg
    • China na Marekani zinatarajiwa kubeba kwa pamoja wajibu kwa dunia

    Siku ya Alhamisi rais Donald Trump wa Marekani alipokutana na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He, aliyeongoza ujumbe wa China katika mazungumzo ya kibiashara ya duru la 9 kati ya China na Marekani, alisema anapenda kuona pande mbili zinafikia makubaliano ya kihistoria ya pande zote mapema iwezekanavyo, hali ambayo si kama tu itazinufaisha Marekani na China, bali pia dunia nzima. Vile vile alipojibu swali la mwandishi wa habari wa Shirika la vyombo vya habari la China CMG. Rais Trump alisema Marekani na China zina wajibu kwa dunia.

    • Hainan yashuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake
    Katika mkutano wa baraza la Boao la Asia uliofanyika mwaka jana mkoani Hainan, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuzidi kulegeza masharti ya soko, kujenga mazingira ya uwekezaji yenye mvuto mkubwa zaidi, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, kuzidi kuongeza manunuzi ya bidhaa kutoka nje, na kuanzisha duru mpya ya ufunguaji mlango zaidi ya China. Baada ya mwaka mmoja, katika mkutano wa mwaka wa baraza hilo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa tena ishara za kufungua mlango zaidi. Hainan ambayo ni dirisha muhimu la sera za ufunguaji mlango na mageuzi katika miaka 40 iliyopita, imeshuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake.
    • China yatoa mapendekezo kwa ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia

    Sherehe ya kufungwa kwa Baraza la usimamizi wa mambo ya dunia kati ya China na Ufaransa ilifanyika jana huko Paris, rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu "kuchangia busara na nguvu katika kuijenga dunia iwe nzuri zaidi", akitoa mapendekezo ya China kuhusu ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia, na kuzitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua halisi katika mambo hayo, na kufanya juhudi za pamoja ili kutimiza kujiamulia mustakabali kwa binadamu.

    • China na Ufaransa zina msimamo wa thamani wa pamoja katika maoni ya usimamizi wa ulimwengu
    Ujenzi wa barabara kuu namba 1 inayounganisha Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo na kituo kikuu cha uchumi Pointe-Noire ulikamilika mwaka 2016, na ulipunguza muda wa safari kati ya miji hiyo miwili kutoka wiki moja hadi saa 6. Barabara kuu hiyo ilijengwa na kampuni ya CSCEC ya China na kusimamiwa na kampuni ya EGIS ya Ufaransa. Baada ya kujengwa kwa barabara kuu hiyo, China na Ufaransa zimeshirikiana tena, China ikiwajibika na ukarabati wa uendeshaji wa barabara na Ufaransa ikishughulikia usimamizi wa uendeshaji huo.
    • Kanuni kadhaa zinastahili kufuatwa katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Ufaransa
    Rais Xi Jinping wa China amesema China na Ufaransa ni marafiki wasio wa kawaida. Kwani Ufaransa ni nchi ya kwanza ya magharibi iliyoanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China, na pia ilitangulia katika kuanzisha ushirikiano na China katika mambo mbalimbali, ikiwemo kuanzisha safari za ndege ya moja kwa moja kati yake na China, kujenga kituo cha utamaduni wa kichina, na kuanzisha idara ya lugha ya kichina katika vyuo vikuu.
    • Rais Xi Jinping wa China kuanza ziara nchini Monaco
    Kutokana na mwaliko wa mfalme Albert Alexandre Louis Pierre Grimaldi wa Monaco, rais Xi Jinping wa China leo anatarajiwa kufika Monaco na kuanza ziara rasmi nchini humo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais wa China kuitembelea nchi hiyo tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1995. Ziara hiyo imetoa ishara wazi duniani kuwa haijalishi kama nchi ni kubwa au ndogo, au ziko umbali wa kiasi gani, zinaweza kuwa wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako