Makamu wa rais wa Sudan Kusini atoa wito wa kufanya mazungumzo ya usuluhishi kuhusu uchaguzi
2024-03-21 08:36:42| cri



Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar amezitaka pande za makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka 2018 zifanye mazungumzo ya usuluhishi kuhusu uchaguzi ujao nchini humo na utungaji wa mpango wa amani.

Bw. Machar amesisitiza haja ya utayari wa kisiasa kati ya pande husika katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa majukumu yaliyosalia kwenye makubaliano hayo ili kutengeneza njia kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi huru, wa haki na kuaminika mwishoni mwa kipindi cha sasa cha mpito ambacho kinamalizika mwezi Februari mwaka ujao.