Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China Mwaka 2024 kufanyika mjini Beijing
2024-08-22 10:20:40| cri

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China kwa Mwaka 2024 (CIFTIS) yatafanyika mjini Beijing katikati ya mwezi Septemba. Kwa mujibu wa mpango kazi, utaratibu wa uandikishaji wa vyombo vya habari utaanza tarehe 21 hadi 29 Agosti.

Wanahabari wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti rasmi ya CIFTIS (www.ciftis.org), na kubonyeza “Kushiriki Maonyesho” na “Uandikishaji wa Vyombo vya Habari” ili kujiandikisha.

Habari kuhusu wakati na njia ya kuchukua kitambulisho kwa wanahabari itatangazwa wakati wengine kwenye ukurasa wa “Kituo cha Habari” ulioko kwenye tovuti rasmi ya CIFTIS.