Kamati Kuu ya CPC yapitisha azimio la kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina
2024-07-19 09:13:52| CRI

Kamati Kuu 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imepitisha azimio la kuimarisha kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina ili kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa kwa umaalumu wa China katika kikao chake cha tatu cha wajumbe wote kilichofanyika mjini Beijing kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi. Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC iliongoza mkutano huo, ambapo katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping alitoa hotuba muhimu.

Katika kikao hicho, Kamati Kuu ilisikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya Ofisi ya Siasa, iliyowasilishwa na Xi kwa niaba ya Ofisi ya Siasa, na kujadili na kupitisha azimio la Kamati Kuu ya CPC kuhusu kuimarisha mageuzi kwa kina ili kuendeleza mambo ya kisasa kwa umaalumu wa China. Xi alitoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu mswada wa azimio hilo.

Taarifa ya mkutano huo iliyotolewa Alhamisi imesema, malengo ya jumla ya kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina ni kuendelea kuboresha na kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China na kuufanya mfumo na uwezo wa utawala wa China kuwa wa kisasa. Haya yote yataweka msingi imara wa kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kisasa ya ujamaa kwa pande zote ifikapo katikati ya karne hii.

Majukumu ya mageuzi yaliyowekwa katika azimio hilo yanatakiwa kukamilika wakati Jamhuri ya Watu wa China inaadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwake mwaka 2029.