Rais wa China ahudhuria mkutano wa SCO+ huko Astana na kutoa hotuba muhimu
2024-07-05 08:43:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai+ (SCO+) huko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan, na kutoa hotuba muhimu iitwayo “Kujenga kwa pamoja nyumba bora zaidi ya SCO”.

Katika hotuba hiyo, rais Xi amesema, hivi sasa mabadiliko katika dunia, zama mpya na ya kihistoria yanajitokeza kwa njia isiyo kawaida, hivyo ni muhimu kuimarisha wazo la kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja, kushikilia kithabiti njia inayojiendeleza ambayo inalingana na hali halisi ya nchi na kanda husika, ili kuijenga SCO iwe bora zaidi, na kuwawezesha watu wa nchi mbalimbali kuishi kwa amani, kufanya kazi kwa furaha na kustawi.

Rais Xi pia ametoa mapendekezo matano, ambayo ni kujenga nyumba ya pamoja ya kushikamana na kuaminiana, nyumba ya pamoja yenye amani na usalama, nyumba ya pamoja yenye ustawi na maendeleo, nyumba ya pamoja yenye ujirani mwema, na kujenga nyumba ya pamoja yenye haki na usawa.