10: Kisiwa cha Taiwan

Hali ya ujumla ya Taiwan

Hali ya kijioglafia:

Taiwan ni mkoa mmoja wa China unaoundwa na visiwa kadhaa kwenye ukingo wa kusini mashariki ya rasi ya China. Mkoa huo unaundwa na Kisiwa cha Taiwan na visiwa vilivyo karibu nacho pamoja na Visiwa vya Penghu, kwa jumla kuna visiwa zaidi ya 80. Eneo la jumla la nchi kavu ni kilomita za mraba elfu 36.

Taiwan inakaribiana na Bahari ya mashariki, kaskazini mashariki yake inapakana na visiwa vya Ryukyu; mashariki yake inakaribia Bahari ya Pasifiki; kusini inapakana na Mlango wa bahari wa Bashi, ambao unapakana na nchi ya Philipines; magharibi yake inatazamana na mkoa wa Fujian wa China bara, katikati ni Mlango wa bahari wa Taiwan, umbali kati ya sehemu zilizo karibu kabisa kati ya pande hizo mbili ni kilomita 130 tu. Mkoa huo mzima uko katikati ya njia ya usafiri kwenye Bahari ya Pasifiki ya magharibi, hivyo hadhi yake ya kimkakati ni muhimu sana.

Mlango wa bahari wa Taiwan

Mlango wa bahari wa Taiwan una urefu wa kilomita 380 toka kusini hadi kaskazini, na wastani wa upana wake toka mashariki hadi magharibi ni kilomita 190, na upana wa sehemu nyembamba kabisa toka Xinzhu ya Taiwan hadi Pingtan ya Fujian ni kilomita 130 tu. Kila ifikapo siku yenye hali ya hewa nzuri, watu wa pwani wa Mkoa wa Fujian wa China bara wakipanda juu kuangalia mbali wataona mawingu na umande kwenye milima mikubwa ya Taiwan, hata wanaweza kuona Mlima Jilong wa kaskazini ya Taiwan.

Hali ya mwinuko wa ardhi na Sura ya ardhi

Eneo la Kisiwa cha Taiwan linachukua zaidi ya 97 % ya eneo la mkoa huo mzima, kisiwa hicho ni kikubwa cha kwanza cha China. Kwenye kisiwa cha Taiwan kuna milima mingi, na eneo la milima mirefu na midogo linachukua theluthi mbili, na eneo la tambarare ni chini ya theluthi moja. Milima Zhongyang, Milima Yushan, Milima Xueshan, Milima Ali na Milima Taidong ni milima mikubwa mitano kwenye kisiwa hicho. Umaalum wa hali ya mwinuko wa ardhi ya Kisiwa cha Taiwan ni kuwa, katikati imeinuka, na pande mbili ni ya chini, na Milima Zhongyang inayoanzia kusini hadi kaskazini ni kama mstari wa katikati unaotenganisha pande mbili za mashariki na magharibi ambazo zinaelekea chini kwa pwani za bahari. Kilele kikuu Yushan cha Milima Yushan kina mwinuko wa mita 3997 ni kilele kirefu cha kwanza huko Taiwan.

Hali ya hewa na mimea na mazao

Mkoa wa Taiwan uko katikati ya ukanda wa joto na wa fufutende, hali ya hewa ya huko ni ya tropiki na nusu tropiki. Kutokana na kuzungukwa na bahari kwa pande nne, hivyo hali ya hewa ya Kisiwa cha Taiwan ni mwafaka kwa kuishi kutokana na pepo za musimu za bahari, katika siku za baridi hakuna baridi kali, na siku za joto hakuna joto kali, wastani wa joto kwa mwaka ni nyuzi 22 sentigredi isipokuwa sehemu ya milima mirefu. Katika sehemu za kawaida, hakuna ukungu na theluji kwa mwaka mzima, mstari wa theluji uko kwenye ukanda wenye mwinuko wa zaidi ya mita 3000 kwenye usawa wa bahari. Katika Kisiwa Taiwan kuna mvua nyingi na kisiwa hicho kinakumbwa na tufani mara kwa mara.

Eneo la misitu la Taiwan linachukua nusu ya eneo la jumla la mkoa huo mzima, na ni kubwa kwa mara moja kuliko eneo la misitu la Uswisi, malimbikizo ya mbao ni zaidi ya mita za ujazo milioni 300. Kutokana na athari ya mabadiliko ya a hali ya hewa, miti ya Taiwan ni ya aina nyingi mbalimbali karibu 4000 ya kanda ya tropiki, nusu tropiki, kanda ya fufudende na kanda ya baridi. Kisiwa cha Taiwan ni kama bustani ya mimea asilia iliyo maarufu sana barani Asia. Eneo la miti ya kiuchumi kisiwani Taiwan linachukua 80 % ya eneo la misitu la huko. Miti ya camphor ya Taiwan inatia fora duniani. Mazao ya camphor na mafuta ya camphor yaliyozalishwa kutoka kwa miti hiyo ni bidhaa muhimu za Taiwan, utoaji wake unachukua 70 % ya ule wa jumla duniani.

Taiwan imezungukwa na bahari kwa pande nne, tena iko katika sehemu ya makutano ya mawimbi ya joto na mawimbi ya baridi, mazao ya baharini ni mengi na ya aina mbalimbali. Kuna aina zaidi ya 500 za samaki. Sehemu za Gaoxiong, Jilong, Suao, Hualian, Xingan, na Penghu ni sehemu maarufu za uvuvi. Aidha, chumvi za bahari zilizozalishwa na Taiwan pia zinajulikana tangu enzi na dahari.


1 2 3 4 5 6 7 8