Hali ilivyo ya sasa ya maingiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande mbili
Katika miaka 30 toka mwaka 1949 hadi 1978, kutokana na mapambano makali ya kijeshi na hali wasiwasi ya kukabiliana kijeshi kwenye sehemu ya Mlango wa bahari wa Taiwan, mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili yalikomeshwa kimsingi, ambapo aina chache tu za bidhaa za mahitaji ya lazima kama vile dawa za mitishamba za China bara na nyinginezo zilisafirishwa hadi Taiwan kwa kupitia Hongkong, tena kiasi cha bidhaa hizo zilizosafirishwa ni kidogo.
Baada ya mwaka 1979, serikali ya China ilichukua hatua kadha wa kadha za kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi kati ya China bara na Taiwan, ambapo utawala wa Taiwan pia ulikuwa hauna njia nyingine ila tu kurekebisha sera yake ya kiuchumi na kibiashara inayohusika na China bara, na ulilegeza vizuizi vya mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba, 2003, thamani ya jumla ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola za kimarekani bilioni 309.18, miongoni mwake, thamani ya bidhaa zilizouzwa na China bara kwenye soko la Taiwan ilifikia dola za kimarekani bilioni 48.89, na thamani ya bidhaa zilizoagizwa na China bara kutoka Taiwan ilifikia dola za kimarekani bilioni 260.29, ambapo pengo la biashara lilifikia dola za kimarekani bilioni 211.4. Kuanzia mwaka 1991, China bara imekuwa chanzo kikuu cha urari kwa Taiwan. Wakati huo huo Taiwan ikawa moja kati ya sehemu zilizowekeza vitega uchumi vingi China bara.
Hivi sasa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China bara na Taiwan umeendelea katika hali maalum kama zifuatazo: Kwanza, uhusiano wa kiuchumi wa pande hizo mbili, kimsingi ni biashara isiyo ya moja kwa moja na wafanyabiashara wa Taiwan wanawekeza vitega uchumi kwenye China bara, pamoja na kuanzisha viwanda au mashirika halisi, kufanya mangiliano ya kisayansi na kiteknolojia, maingiliano ya kifedha na kutoa mafunzo kwa watu. Pili, kutokana na vizuizi vya utawala wa Taiwan, wafanyabiashara wa Taiwan bado wanawekeza vitega uchumi kwenye China bara kwa njia isiyo moja kwa moja, yaani wakitaka kuwekeza kwenye China bara wanapaswa kupitia kampuni zilizosajiriwa kwenye sehemu ya tatu, na wakiwekeza vitega uchumi chini ya dola za milioni moja wanaweza kupitia kampuni za Taiwan moja kwa moja, lakini vitega uchumi hivyo vinapaswa kuingia China bara kupitia sehemu ya tatu. Kutokana na utawala wa Taiwan kukataa mawasiliano ya moja kwa moja ya biashara na China bara, hivyo biashara ya pande hizo mbili pia inaweza kufanyika kwa kupitia sehemu ya tatu. Na kutokana na utawala wa Taiwan kupiga marufuku uwekezaji wa China bara Kisiwani Taiwan, kumekuwepo kwa hali isiyo ya kawaida na biashara isiyo ya uwiano kati ya pande hizo mbili. Tatu, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa kiuchumi wa kutegemeana wa pande hizo mbili unaimarishwa siku hadi siku, na hali ya kusaidiana na kunufaishana inaonekana dhahiri siku hadi siku.
Mawasiliano ya posta, biashara na usafiri kati ya pande mbili
Mwaka 1979, Serikali ya China ilipendekeza kutimiza mawasiliano ya moja kwa moja katika sekta za posta, biashara na usafiri, zaidi ya miaka 20 iliyopita, serikali ya China imefanya juhudi zisizolegea kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano hayo.
Hali ya maendeleo ya hivi sasa ya mawasiliano hayo kati ya China bara na Taiwan:
Mawasiliano ya posta
Mwaka 1993, Shirikisho la uhusiano wa pande mbili za Mlango wa bahari na Mfuko wa maingiliano yalisaini "Makubaliano kuhusu kuuliza juu ya barua za rejesta na fidia kati ya pande hizo mbili", na idara za posta za pande hizo mbili zilianza rasmi shughuli za barua za rejesta.
Mwaka 1996, Idara ya posta ya China na Idara ya posta ya Taiwan zilianzisha shughuli za moja kwa moja za posta. Kwa kupitia mabomba ya mwanga yaliyojengwa na kukamilika mwaka 1999 na 2000 kati ya China na Marekani, Asia na Ulaya, na Asia na Pasifiki, njia ya moja kwa moja ya mawasiliano ya posta ilijengwa kati ya China bara na Taiwan. Idara za posta za pande hizo mbili zimeanzisha shughuli za simu, mawasiliano ya tarakimu, simu za mkononi, simu za kupitia televisheni na kadhalika.
Mawasiliano ya usafiri
Mwezi Aprili, 1997, majaribio ya usafiri wa moja kwa moja baharini kati ya Fuzhou na Xiamen za China bara na Gaoxiong ya Taiwan yalianzishwa. Mwanzoni mwa mwaka 2001, kutokana na mahitaji ya wakazi wa Jinmen na Mazu, China bara ilifanya juhudi kadiri iwezavyo kutoa msaada wa usafiri baharini kati ya sehemu hizo mbili za Taiwan na sehemu za pwani za mkoa wa Fujian, China. Meli zilizotumia mitaji ya pande hizo mbili na zilizosajiliwa kwenye pande hizo mbili zinachukua njia ya kupeperusha bendera za kampuni zao tu kushughulikia usafirishaji wa abiria na bidhaa kwenye bahari kati ya pande hizo mbili.
Mwezi Desemba, 1995, na mwezi Agosti, 1996, Kampuni ya usafiri wa ndege ya Makau, Kampuni ya usafiri wa ndege ya Jiulong ya Hong Kong zilianzisha njia za safari kati ya Makau na Taiwan, na kati ya Hongkong na Taiwan, ambapo mawasiliano ya usafiri usio wa moja kwa moja kati ya China bara na Taiwan ulianzishwa. Mwaka 2003, wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, ili kurahisisha wafanyabiashara wa Taiwan wanaofanya shughuli zao China bara kurudi nyumbani kwa kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, China bara ilichukua njia ya unyumbufu na kufuata hali halisi, kukubali kampuni 6 za safiri za ndege za Taiwan kutuma ndege kuwachukua mara 16 wafanyabiashara wa Taiwan wasafiri kati ya Taibei na Gaoxiong za Taiwan na Shanghai ya China kwa kupitia kutua Hongkong na Makau.
Mawasiliano ya biashara
Kuanzia mwaka 1979, China bara ikaanza kufungua soko kwa bidhaa za Taiwan, na kuzipa sera nafuu ya kusamehe ushuru au kupunguza ushuru. Mwaka 1978, thamani ya biashara ya pande hizo mbili ilikuwa dola za kimarekani milioni 46, na iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 58.3 mwaka 2003. Kutokana na takwimu zilizotolewa mwaka 2002, China bara imekuwa soko kubwa la kwanza kwa bidhaa za Taiwan zinazouzwa nje, na Taiwan ni soko kubwa la pili la kuingiza bidhaa kwa China bara.
Idara husika mbalimbali na sehemu mbalimbali za China bara zimefanya juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji siku hadi siku, na kutoa huduma bora kwa ndugu wa Taiwan, juhudi hizo zimehimiza uwekezaji wa vitega uchumi wa ndugu wa Taiwan. Hadi mwishoni mwa mwaka 2003, China bara iliidhinisha miradi elfu 60 iliyokwekezwa na wafanyabiasha wa Taiwan, kihalisi, utumiaji wa vitega uchumi vya ndugu wa Taiwan umefikia dola za kimarekani bilioni 58.3. Kuanzia mwaka 1993, China bara imekuwa sehemu waliyochagua kwanza wafanyabiashara wa Taiwan kuwekeza vitega uchumi. Hivi sasa benki 10 zenye mitaji ya Taiwan zimeanzisha ofisi zao China bara, na benki hizo nyingi zimeanzisha vituo vyao mjini Shanghai au mjini Beijing.
Lakini mawasiliano ya posta, biashara na usafiri kati ya China bara na Taiwan bado yanafanyika katika hali isiyo ya moja kwa moja, au kwa upande mmoja au katika sehemu kadhaa tu.
Na vifurushi vya pande hizo mbili bado vinapaswa kupelekwa kwa kupitia Hongkong na Makau, na shughuli nyingine za aina mbalimbali kwenye posta bado hazijaweza kuanzishwa.
Mpaka sasa safari za ndege bado hazijaweza kufanyika moja kwa moja kati ya China bara na Taiwan; wasafiri wa pande hizo mbili wanapaswa kupitia Hongkong na Makau; safari za moja kwa moja za majaribio bado ni za abiria tu, hazijafikia kwenye bidhaa za biashara kati ya pande hizo mbili, na bidhaa za biashara kati ya pande hizo mbili bado zinapaswa kupitia sehemu ya tatu ya Japan au Hongkong.
Soko la China bara limefunguliwa kwa mashirika yote na bidhaa zote za Taiwan, lakini bidhaa za China bara zinazosafirishwa kwa Taiwan bado zinazuiliwa kwa hali mbalimbali za ubaguzi na Taiwan, bidhaa nyingi bora za China bara au zinazohitajiwa sana na ndugu wa Taiwan bado hazijaweza kuingia Taiwan; mashirika ya China bara bado hayajaruhusiwa kuwekeza vitega uchumi huko Taiwan, mashirika ya biashara ya lazima pia hayajaruhusiwa kuanzishwa huko Taiwan; ni vigumu kwa mashirika ya China bara kuanzisha au kushiriki maonesho au mazungumzo ya biashara huko Taiwan; hata watu wanaoshughulikia mambo ya uchumi na biashara wakitaka kwenda Taiwan kufanya ukaguzi au matembezi pia hukutana na vizuizi vingi.
|