Idadi ya watu na makabila
Idadi ya watu
Sehemu ya Taiwan ina idadi kubwa ya watu na mashamba machache. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2001, idadi ya jumla ya watu wa Taiwan ilikuwa milioni 22.4, na kila eneo la kilomita moja za mraba kuna watu 619.
Uwiano wa umri wa idadi ya watu wa Taiwan unaelekea kuwa na wazee wengi. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2001, idadi ya watu wenye umri wa miaka 0 hadi 14 ilipungua na kufikia 25.8 %, na idadi ya watu wenye umri wa miaka 15 hadi 64 iliongezeka na kufikia 67.4 %, na idadi ya watu wenye umri wa miaka zaidi ya 65 iliongezeka na kufikia 6.8 %.
Msongamano wa watu kisiwani Taiwan hauna uwiano. Eneo la milimani linalochukua theluthi moja ya eneo la jumla la Taiwan lenye mwinuko wa zaidi ya mita 1000, kwa wastani kila eneo la kilomita moja za mraba lina watu zaidi ya 20 tu. Na katika miji ya Taiwan kila eneo la kilomita moja za mraba kuna watu zaidi ya 4800, hasa katika miji ya Taibei, Gaoxiung, Taizhong, Jilong, Xinzhu, Jiayi na Taiwan, msongamano wa watu ni mkubwa zaidi, na eneo la miji hiyo 7 linachukua 2.9 tu la lile la jumla la Taiwan, lakini idadi ya watu inachukua 31 % ya ile ya jumla ya Taiwan.
Sera ya idadi ya watu ya Taiwan inarekebishwa mara kwa mara kutokana na maendeleo ya jamii na uchumi. Kuanzia mwaka 1965, Taiwan ilianza kutekeleza "mpango wa familia", pamoja na vizuizi kuhusu umri wa miaka ya kufunga ndoa kwa vijana na umri wa miaka ya uzazi, sera hiyo inatetea kuwa "mume na mke wakizaa mtoto mmoja siyo kidogo, lakini wakizaa watoto wawili ni mwafaka kabisa". Baadaye, kiwango cha uzazi wa kina mana wenye umri wa kuzaa watoto kilipungua siku hadi siku, hii imechangia kwa kiasi fulani kupunguza ongezeko la idadi ya watu. Lakini kupunguza kwa ongezeko la idadi ya watu kulisababisha kuongezeka kwa idadi ya wazee na kupunguza kwa nguvukazi. Hivyo utawala wa Taiwan ulirekebisha "sera na mwongozo wa idadi ya watu" mwaka 1990, na kutoa sera ya "kuzaa watoto wawili ni mwafaka, hata kuzaa watoto watatu siyo wengi". Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Taiwan umechukua zaidi sera ya kuhamasisha watu wazae watoto.
Makabila
Taiwan ni sehemu yenye makabila mengi kama vile wahan, wamongolia, wahui, wamiao na wagaoshan. Miongoni mwao zaidi ya 97 % ya watu wa huko ni wahan. Na miongoni mwa idadi ya watu wa kabila la wahan, watu wa sehemu ya Minnan na Kejia ni wengi zaidi. Waminnan walikuwa wazawa wengi zaidi wa Quanzhou na Zhangzhou wa Mkoa wa Fujian, na wakejia walikuwa wazawa wa Meizhou na Chaozhou wa Mkoa wa Guangdong.
Kabila la wagaoshan ni kabila dogo muhimu la Taiwan. Kuhusu chanzo cha kabila la wagaoshan la Taiwan kuna maoni tofauti, lakini utafiti mwingi zaidi umeonesha kuwa, mababu wa kabila la wagaoshan walihamia Taiwan kutoka China bara. Kabila la wagaoshan la Taiwan ni pamoja na wagaoshan wa tambarare na wa sehemu ya milimani. Idadi ya jumla ya wagaoshan inaongezeka siku zote, ilipofika mwaka 2001, idadi ya jumla ya wagaoshan wa Taiwan ilifikia laki 4.15.
Kabila la wagaoshan la Taiwan ni pamoja na waamei, wataiya, wapaiwan, wabuyi, wabeinan, walukai, wazou, wayamei, wasaixia na washao (mwanzoni ni wacao).
|