10: Kisiwa cha Taiwan

Chanzo cha suala la Taiwan

Baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, Taiwan ilirudishwa kwa China kisheria na kihalisi kutokana na ukweli wa mambo. Lakini baadaye kuwepo tena kwa suala la Taiwan ni kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanzishwa na Chama cha Guomintang cha China, na sababu kubwa zaidi ni kutokana uingiliaji kati wa nguvu za nje.

Suala la Taiwan na vita vya ndani vilizoanzishwa na Chama cha Guomintang

Wakati wa mapambano yaliyofanywa na China dhidi ya uvamizi wa Japan, Chama cha Guomintang cha China na Chama cha kikomunisti cha China vilianzisha muungano wa kitaifa wa kupambana na uvamizi wa ubeberu wa Japan. Baada ya kushinda katika vita hivyo, kundi la Chama cha Guomintang lililoongozwa na Jiang Keishek lilitegemea uungaji mkono wa Marekani, likaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kote nchini. Chama cha kikomunisti cha China kiliwaongoza wananchi wa China kufanya mapigano ya ukombozi kwa zaidi ya miaka mitatu, ambapo kundi la Chama cha Guomintang lililofanya ufisadi na kwenda kinyume na nia ya wananchi lilichukizwa na wananchi wa makabila mbalimali wa nchi nzima, serikali ya "Jamhuri ya China" ya Chama cha Guomintang ilipinduliwa. Tarehe 1 Oktoba, 1949, Jamhuri ya Watu wa China ilianzishwa na kuwa serikali pekee halali ya China. Maofisa kadhaa wa kundi la Chama cha Guomintang walikwenda Taiwan na kuikalia, wakisaidiwa na serikali ya Marekani ya wakati huo wakazifanya pande mbili za Mlango wa bahari wa Taiwan zikae katika hali ya kutenganishwa.

Suala la Taiwan na Jukumu la serikali ya Marekani

Baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, katika hali ambayo kambi mbili kubwa zenye nguvu za mashariki na maghabiri zilikabiliana, kutokana na mikakati yake ya dunia nzima na kuzingatia kulinda maslahi yake yenyewe, serikali ya Marekani ilifanya chini juu kutoa fedha, silaha na kutuma watu kuunga mkono kundi la Chama cha Guomintang kufanya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini China, na kujaribu kuangamiza Chama cha kikomunisti cha China. Lakini hatimaye serikali ya Marekani ilishindwa kutimiza lengo lake.

Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, serikali ya Marekani ilichukua sera ya kuifanya China kukaa katika hali ya upweke na kuizuia, hata baada ya kuanzishwa kwa vita dhidi ya Korea ya kaskazini, iliingilia kati kijeshi uhusiano wa pande mbili za Mlango wa Bahari wa Taiwan, uhusiano ambao ni mambo matupu ya ndani. Mwaka 1950, kikosi cha 7 cha manuari za Marekani kilivamia Mlango wa bahari wa Taiwan, na kikosi cha 13 cha ndege cha Marekani kilikalia Taiwan. Mwezi Desemba mwaka 1954, Marekani iliwekeana na utawala wa Taiwan ati "Mkataba wa ulinzi wa pamoja", ikauweka mkoa wa Taiwan wa China kwenye "ulinzi" wa Marekani. Sera ya makosa ya serikali ya Marekani ya kuendelea kuingilia kati mambo ya ndani ya China ilisababisha hali wasiwasi na hali ya kukabiliana kwa muda mrefu kwenye sehemu ya Mlango wa bahari wa Taiwan, tangu hapo suala la Taiwan ikawa mgogoro mkubwa kati ya China na Marekani.

Kutokana na maendeleo na mabadiliko ya hali ya kimataifa na ukuaji wa China mpya, Marekani ikaanza kurekebisha sera yake juu ya China, ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukaanza kuelekea kuwa wa kawaida. Mwezi Oktoba mwaka 1971, Mkutano wa 26 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la No.2758 la kurudisha haki zote halali za Jamhuri ya watu wa China katika Umoja wa Mataifa na kumfukuza "mwakilishi" wa utawala wa Taiwan. Mwezi Februali wa mwaka 1972, rais Richard Nixon wa Marekani aliitembelea China, ambapo China na Marekani zilitoa taarifa ya pamoja huko Shanghai, China. Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa: "Marekani imetambua kuwa, wachina wote walioko pande mbili za Mlango wa Bahari wa Taiwan wanaona kuwa iko China moja tu duniani, Taiwan ni sehemu moja ya China. Serikali ya Marekani haitoi maoni tofauti juu ya msimamo huo."

Mwezi Desemba, 1978, serikali ya Marekani ilikubali kanuni tatu za kuanzisha uhusiano wa kibalozi zilizotolewa na serikali ya China, yaani Marekani isimamishe "uhusiano wa kibalozi" na utawala wa Taiwan, ifute "Mkataba wa ulinzi wa pamoja" na kuondoa jeshi lake kutoka Taiwan. Nchi mbili China na Marekani ziliwekeana rasmi uhusiano wa kibalozi kuanzia Tarehe 1 Januari, 1979. Taarifa ya pamoja ya China na Marekani kuhusu kuwekeana uhusiano wa kibalozi ilisema kuwa, "Marekani inatambua serikali ya Jamhuri ya watu wa China ni serikali halali pekee ya China. Ndani ya eneo hilo, wananchi wa Marekani watadumisha mawasiliano ya kiutamaduni, kibiashara na mengine yasiyo ya kiserikali na watu wa Taiwan"; "Serikali ya Marekani inatambua msimamo wa China yaani kuwepo kwa China moja tu, Taiwan ni sehemu moja ya China".

Lakini jambo linasikitisha ni kuwa, ilikuwa haijafikia miezi mitatu tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, Bunge la Marekani lilifika hadi kupitisha "Sheria kuhusu uhusiano na Taiwan", na sheria hiyo ilisainiwa na rais wa Marekani ikaanza kufanya kazi. Sheria hiyo iliwekwa kanuni nyingi zinazokiuka Taarifa ya China na Marekani ya kuwekeana uhusiano wa kibalozi na kanuni za sheria ya kimataifa. Serikali ya Marekani ikifuata sheria hiyo ikaendelea kuiuzia Taiwan silaha na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, na kuzuia muungano wa Taiwan na China bara.

Ili kutatua suala kuhusu Marekani kuiuzia Taiwai silaha, serikali za China na Marekani zilifanya mazungumzo na kufikia makubaliano tarehe 17, Agosti, 1982, ambapo zilitoa taarifa ya tatu ya pamoja kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani. Katika taarifa hiyo, serikali ya Marekani ilisema kuwa Marekani haitafuti kutekeleza sera moja ya kuiuzia Taiwan silaha kwa muda mrefu, uwezo na kiasi cha silaha inazoiuzia Taiwan hakipaswi kuzidi kiwango cha silaha zile ilizoiuzia katika miaka kadhaa baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, na Marekani iko tayari kupunguza hatua kwa hatua silaha inazoiuzia Taiwan, ili kupata ufumbuzi wa mwisho wa suala hilo baada ya muda. Lakini katika miaka mingi iliyopita, serikali ya Marekani si kama tu haikufuata kwa makini kanuni zilizowekwa kwenye taarifa, bali pia ilifanya vitendo vya kukiuka taarifa mara kwa mara. Mwezi Septemba, 1992, serikali ya Marekani hata iliamua kuiuzia Taiwan ndege za kivita 150 za aina ya F-16 ambazo ni ndege zenye uwezo wa juu. Kitendo hicho cha serikali ya Marekani kiliongeza vikwazo kwa maendeleo y uhusiano kati ya China na Marekani na utatuzi wa suala la Taiwan.

Yote hayo yameonesha kuwa, suala la Taiwan haliwezi kutatuliwa mpaka sasa, serikali ya Marekani inapaswa kuwajibika nalo.


1 2 3 4 5 6 7 8