Historia ya uendelezaji wa Taiwan
Taiwan ni sehemu moja ya China isiyotengeka. Kijioglafia, katika zama za kale sana, Taiwan na China bara zilikuwa ya sehemu moja. Baadaye kutokana na kusogea kwa ardhi, nchi kavu iliyoungana ilizama kuwa mlango wa bahari, Taiwan ikawa kisiwa. Mabaki mengi yaliyofukuliwa katika sehemu mbalimbali za Taiwan kama vile vyombo vya mawe, vyombo vya kauri nyeusi na kauri za rangi yote yameonesha kuwa, utamaduni wa Taiwan wa kabla ya historia ulikuwa na chanzo kimoja na China bara.
Kutokana na kumbukumbu za maandishi ya zama za kale, mwaka 230, mfalme wa dola la Wu Sun Quan aliwahi kumtuma jenerali Wei Wen na Zhu Gezhi kuwaongoza askari wa maji wapatao elfu 10 kuvuka bahari kufika Taiwan. Huu ulikuwa mwanzo kwa wakazi wa China bara kutumia ujuzi wa utamaduni wa kimaendeleo kwa kuendeleza Taiwan. Ilipofika mwishoni mwa karne ya 6 na mwanzoni mwa karne ya 7 wakati wa Enzi ya Sui, Mfalme Suiyangdi aliwatuma watu kwenda Taiwan mara tatu, kufanya ukaguzi, kufahamishwa desturi na mila tofauti na kuwapa pole wakazi wa huko. Baadaye katika muda wa miaka 600 toka Enzi ya Tang hadi Enzi ya Song, wakazi wa pwani ya China bara, hasa wakazi wa sehemu ya Quanzhou na Zhangzhou mkoani Fujian walikimbia au kuhamia Penghu na Taiwan kwa ajili ya kukwepa vurugu za vita, ambapo walifanya shughuli za kilimo huko. Mwaka 1335, Enzi ya Yuan ilianzisha rasmi "Idara ya doria na ukaguzi" huko Penghu, ikasimamia mambo ya raia wa Penghu na Taiwan. Tangu hapo China ilianzisha mamlaka maalum ya utawala huko Taiwan.
Baada ya Enzi ya Ming, mawasiliano kati ya watu wa China bara na Taiwan yaliendelea siku hadi siku. Mwanabaharia Zheng He aliongoza kikosi kikubwa cha merikebu kutembelea nchi mbalimbali za Asia ya kusini mashariki, ambapo waliwahi kukaa huko Taiwan na kuwalepelekea wakazi wa huko vitu vya sanaa na mazao ya kilimo. Mwaka 1628, wakati mkoa wa Fujian ulipokumbwa na maafa makubwa ya ukame, wakazi wa huko walikumbwa na balaa kubwa, mkazi wa Fujian Zheng Zhilong aliwashirikisha watu waliokumbwa na maafa kwenda Taiwan kujihusisha na kilimo na kuzalisha mazao ili kujipatia chakula. Tangu hapo Taiwan ikaingia kipindi cha uendelezaji mkubwa.
Zheng Chenggong arudisha mamlaka ya Taiwan
Baada ya kipindi cha katikati cha karne ya 16, Kisiwa cha Taiwan chenye utajiri wa maliasili kikaanza kuwa shabaha la wakoloni wa magharibi. Mabeberu wa Hispania na Ureno walishambulia Taiwan kwa mfululizo, ama kunyang'anya maliasili, ama kufanya uvamizi wa utamaduni wa kidini, ama kutuma askari kuikalia. Mwaka 1642, waholanzi walinyang'anya vituo vya wahispania katika sehemu ya kaskazini huko Taiwan, tangu hapo Taiwan ikawa sehemu ya koloni la Uholanzi.
Wakoloni wa Uholenzi walipokalia Taiwan waliwanyonya kishenzi watu wa Taiwan. Watu wa Taiwan walipambana na wakoloni wa Uholanzi bila kusita. Mwaka 1662, shujaa wa taifa Zheng Chenggong alikuwa akishirikiana na watu wa Taiwan, aliwafukuza wakoloni wa Uholanzi na kurudisha mamlaka ya Taiwan. Zheng Chenggong alifariki dunia kwa ugonjwa siku chache baadaye. Mtoto wake Zheng Jing na mjukuu wake Zheng Ke kwa nyakati tofauti waliendesha Taiwan kwa miaka 22. Watu wa vizazi vitatu vya ukoo wa Zheng waliposhika madaraka ya utawala wa Taiwan, walitoa motisha kwa shughuli za kutengeneza sukari na chumvi, kuanzisha viwanda na kuendeleza shughuli za biashara, kuanzisha shule, na kuboresha njia za uzalishaji wa jadi za kabila la wagaoshan. Hatua hizo zilisukuma mbele maendeleo ya haraka ya uchumi na utamaduni wa Taiwan. Kipindi hiki kilikuwa kipindi muhimu cha maendeleo katika historia ya Taiwan, ambacho kiliitwa kuwa "Kipindi cha Zheng cha enzi ya Ming".
Taiwan yawekwa kwenye Ramani ya China mwanzoni mwa Enzi ya Qing
Mwaka 1683, serikali ya Enzi ya Qing ilituma jeshi kuishambulia Taiwan, Zheng Ke aliongoza wafuasi wake wote kuitii serikali hiyo. Serikali ya Enzi ya Qing iliweka manispaa moja na wilaya tatu, na kuiweka Taiwan iwe ya Mkoa wa Fujian. Taiwan ikawekwa tena chini ya mamlaka ya utawala wa pamoja wa serikali kuu ya China, na kuwa na uhusiano barabara zaidi na China bara katika sekta za siasa, uchumi na utamduni, na kuwa sehemu moja isiyotengeka ya nchi nzima ya muungano.
Mwaka 1885, serikali ya Enzi ya Qing iliijenga Taiwan kuwa mkoa, na kutuma Liu Mingchuan kuwa mkuu wa kwanza wa mkoa wa Taiwan. Liu Mingchuan aliwahamasisha wakazi wa mikoa ya Fujian na Guangdong kuhamia Taiwan ili kuendeleza Taiwan katika sekta mbalimbali, ambapo zilianzishwa idara kuu ya kilimo, idara kuu ya simu ya upepo, idara kuu ya reli, idara ya silaha, idara ya mawasiliano ya biashara, idara ya madini na mafuta na idara ya ukataji wa miti; kilijengwa kituo cha mizinga, kushughulikia upya mambo ya ulinzi; kuweka nyaya za umeme, kuanzisha idara ya posta; kutandika reli, kuchimba madini, kuunda meli za biashara, kuendeleza viwanda na biashara; kujenga shule za kichina na kiulaya kwa kuendeleza utamaduni na elimu huko Taiwan.
Nusu ya pili ya karne ya 19, Japan ilishika njia ya maendeleo ya kibepari. Mwaka 1894, Japan ilianzisha vita vya China na Japan yaani vita vya Jiawu. Serikali ya Enzi ya Qing iliyoshindwa katika vita hivyo ilisaini "Mkataba wa Maguan" uliodhuru mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, ilitenga Taiwan na visiwa vya Penghu na kuvikabidhi kwa Japan, tangu hapo Taiwan ikawa koloni la Japan, kipindi cha muda mrefu wa miaka 50 cha kukaliwa na Japan kilianzia hapo.
Baada ya kukalia Taiwan, Japan iliweka Jumba la gavana mkuu, yaani mamlaka yake ya kuitawala Taiwan, na pia iliweka ofisi za tarafa na wilaya katika sehemu mbalimbali huko Taiwan, kutekeleza utaratibu wa usimamizi wa polisi na maofisa wa mitaa, kutekeleza utawala wa kikoloni na elimu ya "raia wa mfalme" huko Taiwan. Wakati huo huo, kutokana na mahitaji yake ya kuendeleza uchumi wa nchi yake, mwanzoni Japan iliichukua Taiwan kuwa ni kituo chake cha kuendeleza kilimo na kutengeneza mazao ya kilimo, na kuifanya Taiwan iendeleze hatua kwa hatua viwanda vya utengenezaji na shughuli za mawasiliano na uchukuzi. Katika kipindi cha vita vikuu vya pili vya dunia, ili kufuata sera ya kusonga mbele kwa kuelekea kusini iliyotungwa na wanajeshi waliopenda vita, Japan iliendeleza zaidi viwanda vya aina mbalimbali vilivyohusika na mambo ya kijeshi huko Taiwan.
Kurudishwa na kutenganishwa kwa Taiwan
Kutokana na ukweli wa mambo ya historia, mikataba ya kimataifa iliyosainiwa wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia ilithibitisha tena kuwa Taiwan ni sehemu moja isiyotengeka ya ardhi ya China. Tarehe 1 Desemba, mwaka 1943, "Taarifa ya Cairo" lililosainiwa kati ya China, Marekani na Uingereza ilieleza kuwa, "Ardhi ya China iliyoibwa na Japan kama vile Manjzhou, Taiwan na visiwa vya Penghu zote zirudishwe kwa China". Tarehe 26 Julai, 1945, "Taarifa ya Potsdam" iliyosainiwa na nchi nne za China, Marekani na Uingereza pamoja na Urusi ya zamani ilisisitiza kuwa "masharti yaliyothibitishwa kwenye Taarifa ya Cairo yapaswa kutekelezwa".
Tarehe 15 Agosti, 1945, Japan ilitangaza kupokea vifungu vya "Taarifa ya Potsdam", na kusalimu amri bila masharti yoyote. Tarehe 25 Oktoba, 1945, serikali ya China ilifanya sherehe huko Taibei kupokea usalimishaji wa jeshi la Japan lililokalia mkoani Taiwan. Lakini baada ya kurudishwa kwa Taiwan nchini China, utawala wa wakati huo wa Chama cha Guomintang ulichukua sera ya makosa makubwa, ulitekeleza utawala wa udikteta wa kijeshi, pamoja na ufisadi mkubwa wa maofisa wake, migongano kati ya utawala huo na watu wa Taiwan iliongezeka. Tarehe 28 Februari, 1947, watu wa Taiwan walifanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wa chama cha Guomintang. Chama cha Guomintang kilituma askari wengi kisiwani Taiwan kutoka Jilong kufanya mauaji makubwa, ambapo watu zaidi ya elfu 30 waliuawa. Katika historia tukio hilo liliitwa kuwa "tukio la tarehe 28 Februari".
Tarehe 1 Oktoba, 1949, wananchi wa China walikuwa wakiongozwa na Chama cha kikomunsti cha China walipindua serikali ya Chama cha Guomintang na kutangaza kuzaliwa kwa Jamhuri ya watu wa China. Kabla ya kukombolewa kwa China bara, akina Jiang Keishek , na na baadhi ya maofisa wa serikali na jeshi la Chama cha Guomintang walikwenda Taiwan, ambapo waliitegemea Marekani katika ulinzi na uungaji mkono wake, wakadumisha usalama wa Taiwan na kuzifanya Taiwan na China bara zikae tena katika hali ya kutenganishwa.
|